Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Samia Aomba Kura Wananchi wa Chemba Mkoani Dodoma

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akinadi na Kuomba Kura kwa Wananchi wa Chemba Mkoani Dodoma wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu leo August 31,2025.

Mariam Mwinyi Apokea Milioni 35 za Fomu ya Urais ya Dkt.Mwinyi Kutoka Kwa Uwt

Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amewashukuru Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) pamoja na makundi mbalimbali ikiwemo watu wenye mahitaji maalum na wajane kwa kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kumchangia Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Zanzibar 2025, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Mama Mariam Mwinyi amesema hayo katika hafla maalum ya kumuunga mkono Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi iliyofanyika katika Ukumbi wa Madinat Al Bahr leo, tarehe 29 Agosti 2025. Aidha, Mama Mariam Mwinyi amewapongeza Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuandaa tukio hilo la kumuunga mkono Dkt. Mwinyi kwa kumchangia Shilingi Milioni 35 kwa ajili ya kuchukua fomu kesho katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Vilevile, Mama Mariam Mwinyi amewahimiza wananchi wote kuendelea kudumisha amani na utulivu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba. Naye, Makamu Mwenyekiti wa UWT Zan...

Dkt.Samia aomba kura kwa wananchi wa Chamwino Dodoma

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Chamwino katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho mkoani Dodoma tarehe 31 Agosti, 2025.

Makamu wa Rais Afanya Mazungumzo na Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Zimbabwe

- *TANZANIA NA ZIMBABWE ZAKUBALIANA KUENDELEZA UHUSIANO* Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Kanali Mstaafu Kembo Campbell Mohadi, Mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya siku mbili ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe hapa nchini. Katika siku ya kwanza ya Ziara ya Makamu wa Rais Zimbabwe, viongozi hao wameongoza Ujumbe wa Tanzania na Jamhuri ya Zimbabwe katika mazungumzo rasmi ambayo yamelenga namna ya kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili. Mazungumzo hayo yamegusia zaidi urafiki wa muda mrefu wa kihistoria baina ya Tanzania na Zimbabwe tangu enzi za harakati za ukombozi wa Taifa la Zimbabwe, ambapo Tanzania chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilitoa msaada wa hali na mali kwa wapigania uhuru wa Zimbabwe. Tanzania na Zimbabwe zimekubaliana kuendeleza uhusiano uliopo pamoja na kutunza hist...

Rais Samia Alivyopiga Picha ya 'selfie' na Wananchi wa Kibaigwa

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipiga picha ya 'Selfie' na maelfu ya Wananchi wa Kibaigwa Mkoani Dodoma wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu leo August 30,2025.