Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kilele Maadhimisho ya Miaka 50 ya Tet

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 17, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yanayofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo, Bamaga Jijini Dar es Salaam.  kaulimbiu ya maadhimisho ni _Kitabu Kimoja Mwanafunzi Mmoja, Mpe Kitabu Gusa Ndoto_ .Kaulimbiu hiyo inaunga mkono juhudi za serikali za kuchapa na kusambaza vitabu kwa lengo la kufikia uwiano wa Kitabu kimoja Mwanafunzi mmoja.

Oktoba Kura Zote Kwa Rais Dk. Samia - Ummy Mwalimu

  Na Mwandishi Wetu, TANGA Kazi nzuri na miradi tele ya maendeleo iliyotekelezwa katika Jimbo la Tanga Mjini imetengeneza deni kwa wananchi wa Tanga Mjini dhidi ya Rais Dk. Samia Suluhu ambaye pia ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba, 2025. Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM), Ummy Mwalimu, Juni 16, 2025, alipokuwa akitoa hotuba fupi kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Tanga Mjini katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Tanga. Katika hotuba yake, Ummy Mwalimu amesema Jimbo la Tanga Mjini limepata miradi mingi na mikubwa ya maendeleo ambayo imetatua kero za wananchi.  Kwa msingi huo, Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Dk. Samia kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu, asiwe na wasiwasi wa kura kwani wananchi wa Tanga Mjini watampa asante yao kwa njia ya kumpigia kura nyingi za kishindo ili aendelee kukaa Ikulu awatumikie Watanzania. "Kwa kazi nzuri zilizofany...

Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera Waridhishwa ba Bajeti Kuu ya Serikali

Na Angela Sebastian;Bukoba, Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera ((JWT) imesema kuwa, bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026 iliyosemwa Bungeni na Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba imetoa ufumbuzi wa baadhi ya kero zilizoondoa utulivu wa kubiashara na kudhoofisha mitaji. Hayo yameelezwa na leo mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa huu Nicholaus Basimaki ambapo ameipongeza jitihada za Serikali maana bajeti imegusa maeneo mengi ya wafanyabiashara na itapunguza kero kwao. “Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ameelekeza wasaidizi wake waweze kusikiliza changamoto za wafanyabishara ambapo tumeona kwenye bajeti yameainishwa mambo mbalimbali mfano sheria ya fedha ya serikali za mitaa sura ya 290 ambayo ni hotuba kupitia Waziri wa fedha inapendekeza ifanyiwe maboresho”amesema Basimaki Ameeleza kuwa, wafanyabiashara wanaunga mkono kwamba katika maeneo hayo hasa kwenye maeneo ya tozo na ushuru mfano ushuru wa huduma (service lev) ambayo ilikuwa ikitozw...

Wasira Aeleza Sababu za Ccm,Kuhitajika Milelele

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira ameeleza mambo mbalimbali yanayoifanya CCM kuwa idumu. Mojawapo ya sababu hizo ni wajibu wake wa majukumu endelevu ya kuwatumikia Watanzania. Amesema kutokana na umuhimu wa majukumu hayo kwa ustawi wa nchi na maisha ya Watanzania CCM itakuwepo wakati wote. Wasira ameyasema hayo leo Juni, 16, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita ambako ameanza ziara ya siku tatu ya kukagua uhai wa Chama, kuzungumza na wana CCM na makundi mbalimbali yakiwemo ya viongozi wa dini, wakulima na wafugaji. "CCM ni Chama kikubwa na chenye historia, watu wengi wanadhani CCM ilianza miaka 48 iliyopita, Chama hiki kimerithi mikoba ya vyama vya TANU na Afro Shiraz Party. TANU ina miaka 75 na Afro Shirazi Part y miaka 67. "CCM ni Chama kipya ambacho kimeundwa na vyama vya zamani. Kimekabidhiwa majukumu ya kudumu, hivyo tukisema kidumu Chama Cha Mapinduzi hatuna utani. Tun...

Kampuni Kubwa za Madini Zasaini Mkataba Wa Kuuzia Dhahabu Benki Kuu Tanzania(Bot)

▪️Rais Samia apongezwa kwa maono ▪️Kampuni za GGM,Shanta na Buckreef kuuza Dhahabu kwa BOT,GGR kusafirisha dhahabu. ▪️BOT yanunua Tani 5 ya dhahabu  ▪️Waziri Mavunde apongezwa kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Madini ▪️Tanzania kuingia 10 bora kwa nchi zenye hifadhi kubwa ya Dhahabu Afrika Dodoma Benki ya Tanzania(BOT) leo imesaini mikataba na Kampuni za Uchimbaji Madini za Geita Gold Mine(GGM),Buckreef Gold Ltd na Shanta Ltd juu kampuni hizo kuiuzia BOT kiasi kisichopungua asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa kama ambayo imeelezwa kwenye kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini,Sura ya 123. Hafla hiyo ya utiaji saini mikataba ya uuzwaji wa dhahabu imefanyika leo tarehe 16.06.2025 Jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu L. Nchemba na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde. Akizungumza katika hafla hiyo Mh.Mwigulu Nchemba amempongeza Mh. Rais Dkt. SamiaS. Hassan kwa uongozi wenye maono na ambao umechochea kukua kwa hifadhi ya dhahabu ya BOT hali ambayo itasaidia kuimaris...

Rea Kuendelea Kuwezesha Waendelezaji wa Miradi ya Nishati Vijijini

📌RC Njombe apongeza usimamizi wa miradi ya REA Wakala wa Nishati Vijijini (REA) utaendelea kutoa sapoti kwa waendelezaji wa miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme kote nchini ili kuwezesha wananchi wengi kufikiwa na huduma bora ya nishati ambayo inachangia kuinua uchumi wa wananchi pamoja na huduma za  kijamii.  Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amebainisha hayo Mkoani Njombe Juni 17, 2025 kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony Mtaka alipofika ofisini kwake kuelezea ziara yake ya kukagua miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme mkoani humo.  "Njombe ni moja ya Mkoa ambayo imepokea sapoti kubwa kwenye uendelezaji wa miradi ya nishati jadidifu," alisema Mhe. Balozi Kingu. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Mtaka alimueleza Mhe. Balozi Kingu namna ambavyo anafarijika kwa sapoti inayotolewa na REA kwenye miradi hiyo na alisema kwa namna mkoa huo ulivyo bado zipo fursa nyingi za kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji ya mito. "Jio...