WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Ajira na Mahusiono Deus Sangu amesema wakati sekta ya madini ikiendelea kung'aa kwa kuchangia takriban asilimia 10.1 ya Pato la Taifa na kuajiri maelfu ya Watanzania, kuna shujaa mmoja ambaye ni Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi(WCF) anahakikisha jasho la mfanyakazi huyo haliendi bure anapopatwa na janga.
Akizungumza kwenye Banda la Mfuko huo Leo Septemba 24,2024 Katika maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teklojia ya Madini yanayofanyika Katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan yanayofanyika Mkoa wa Geita ameeleza kwamba ndani ya miaka 10 ya WCF imejijenga kuwa
mkombozi wa kweli kwa wafanyakazi wa migodini na sekta nyingine zote.
Aidha ameeleza kwamba Mfuko huu unatoa fidia kwa mfanyakazi anapopata ajali kazini, anapougua ugonjwa unaotokana na kazi, au kwa wategemezi wake mwenza na watoto pindi mfanyakazi anapofariki dunia akiwa kazini.
Aidha Katika kipindi Cha rais wa awamu ya sita mufuko ulikuwa na Bilioni 770 na mpaka Sasa kufikia Trilioni 1.1 Mafanikio ya WCF hayawezi kuelezewa bila kutaja mageuzi ya kiuchumi chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Thamani ya Mfuko imekua kwa kasi ya hadi kutoka Shilingi Bilioni 770 hadi kufikia zaidi ya Shilingi Trilioni 1.1 . Hii ni ishara kuwa mfuko upo imara na tayari kulipa fidia wakati wowote bila kuchelewa
Zamani madai ya fidia yalichukua miezi. Leo, hadithi ni tofauti.
WCF imeboresha mifumo yake ya TEHAMA kwa asilimia 99. Madai yote, malalamiko na uhakiki sasa unafanyika kidijitali hakuna makaratasi, hakuna foleni. Mfanyakazi anayepata ajali Geita anaweza kuwasilisha dai lake akiwa hapo hapo mgodini na kulipwa kwa wakati.
Ameongeza Kwa kutoka wito Kwa waajirii wote nchini ambao bado hawajajiunga na mfuko huo kwamba kutokujisajili WCF ni sawa na kumuacha mfanyakazi wako bila kofia ngumu ya kisheria. Sheria inataka kila mwajiri amlinde mfanyakazi wake.
Vilevile, WCF imehimizwa kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wafanyakazi ili kila mmoja ajue haki yake kwamba akipata ajali, ugonjwa au mauti ya kazini, kuna mfuko imara wa Trilioni 1.1 uliosimama kwa ajili yake na familia yake.
Mwisho


Comments
Post a Comment