Na Mwandishi Wetu BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeandaa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wasimamizi na waendeshaji wa matukio nchini kama hatua ya kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria za nchi ili waweze kukuza ubora na viwango vya kitaalamu katika sekta ya matukio. Mafunzo haya yanalenga kuwafikia wadau mbalimbali, wakiwemo Watangazaji na Waongozaji wa Matukio (MCs), Maafisa Utamaduni, Maafisa Habari, Promota, kampuni zinazojihusisha na uandaaji na usimamizi wa matukio pamoja na wadau wengine katika sekta hiyo. Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASARA, Amosi Mazaba, alisema mafunzo hayo yatafanyika tarehe 23 – 24 Novemba 2026 katika ukumbi wa The East Africa Commercial and Logistics Centre (EACLC), Ubungo, Dar es Salaam. Iliyokuwa standi ya Mabasi ya Mikoani Ubungo. Aidha, alisema mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za BASATA za kuimarisha weledi, ujuzi na mifumo ya uendeshaji na usim...
Marato tv - Sauti ya Jamii