MBUNGE wa Jimbo la Musoma Mjini, Mhe. Mgore Miraji Kigera, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mjumbe wa Bodi ya TRC, Mkurugenzi wa LATRA pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wamepata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa Msimamizi wa Kampuni ya FS Engineering Company, Mhandisi Salvatore, kuhusu mafanikio na uzoefu wa kampuni hiyo katika sekta ya usafiri na usafirishaji wa makontena ndani ya nchi saba za Bara la Ulaya.
Katika maelezo hayo, wamepata fursa ya kufahamu uzoefu, mifumo ya kiutendaji na utaalamu wa kampuni hiyo katika kuendeleza huduma za usafiri wa reli na usafirishaji wa mizigo, hususan makontena, kwa kuzingatia viwango na teknolojia za kisasa.
FS Engineering Company ni miongoni mwa kampuni zilizoshirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), kupitia makubaliano ya ushirikiano, ambapo pia imetoa ushauri wa kitaalamu na kiufundi katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) katika kipande cha Dar esSalaam–Morogoro–Makutupora.
Uzoefu huo wa kimataifa unatoa fursa muhimu ya kujifunza na kubadilishana maarifa yanayoweza kuchochea maboresho ya sekta ya usafiri na usafirishaji nchini, kuongeza ufanisi wa huduma za reli na kuimarisha ushindani wa Tanzania katika sekta ya usafirishaji wa mizigo

Comments
Post a Comment