Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

BASATA YAJIPANGA KUWANOA WASIMAMIZI NA WAENDESHA MATUKIO

  Na Mwandishi Wetu BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeandaa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wasimamizi na waendeshaji wa matukio nchini kama hatua ya kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria za nchi ili waweze kukuza ubora na viwango vya kitaalamu katika sekta ya matukio. Mafunzo haya yanalenga kuwafikia wadau mbalimbali, wakiwemo Watangazaji na Waongozaji wa Matukio (MCs), Maafisa Utamaduni, Maafisa Habari, Promota, kampuni zinazojihusisha na uandaaji na usimamizi wa matukio pamoja na wadau wengine katika sekta hiyo. Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASARA, Amosi Mazaba, alisema mafunzo hayo yatafanyika tarehe 23 – 24 Novemba 2026 katika ukumbi wa The East Africa Commercial and Logistics Centre (EACLC), Ubungo, Dar es Salaam. Iliyokuwa standi ya Mabasi ya Mikoani Ubungo. Aidha, alisema mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za BASATA za kuimarisha weledi, ujuzi na mifumo ya uendeshaji na usim...

MBUNGE MGORE:UZOEFU WA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA UTAIMARISHA SEKTA YA USAFIRI NA USAFIRISHAJI

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Mjini, Mhe. Mgore Miraji Kigera, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mjumbe wa Bodi ya TRC, Mkurugenzi wa LATRA pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wamepata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa Msimamizi wa Kampuni ya FS Engineering Company, Mhandisi Salvatore, kuhusu mafanikio na uzoefu wa kampuni hiyo katika sekta ya usafiri na usafirishaji wa makontena ndani ya nchi saba za Bara la Ulaya. Katika maelezo hayo, wamepata fursa ya kufahamu uzoefu, mifumo ya kiutendaji na utaalamu wa kampuni hiyo katika kuendeleza huduma za usafiri wa reli na usafirishaji wa mizigo, hususan makontena, kwa kuzingatia viwango na teknolojia za kisasa. FS Engineering Company ni miongoni mwa kampuni zilizoshirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), kupitia makubaliano ya ushirikiano, ambapo pia imetoa ushauri wa kitaalamu na kiufundi katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) katika kipande cha Dar esSala...

WAKAZI WA KISIWA CHA KAMASI WAASWA KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME

  *WAKAZI WA KISIWA CHA KAMASI WAASWA KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME* 📌 *Nishati ya uhakika ni msingi wa uchumi imara, huduma bora za kijamii na maendeleo endelevu.* 📍 *Kamasi, Ukerewe – Mwanza* Wakazi wa Kisiwa cha Kamasi kilichopo katika Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza, wamehimizwa kutumia fursa ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa kujitokeza na kujiunga na huduma hiyo ili kuongeza tija katika shughuli zao za kila siku, kukuza shughuli za kiuchumi na kuboresha ustawi wa jamii. Wito huo umetolewa na wataalamu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Kampuni ya Volt Afrika Limited pamoja na viongozi wa Serikali katika ngazi ya vitongoji na vijiji, waliofika kisiwani humo kwa ajili ya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na kutumia huduma ya umeme kupitia mradi wa umeme jua unaotekelezwa katika eneo hilo. Katika zoezi hilo la uhamasishaji, wananchi wameelezwa namna umeme unavyoweza kuwa kichocheo cha mabadiliko ya kiuchumi kwa kuwawezesha kuanzisha na kue...

DKT. MWAMBA:UBORA WA ISO 9001:2015 ULETE MATOKEO CHANYA KATIKA HUDUMA ZA BIMA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha cheti cha kimataifa cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 kinatafsiriwa katika maboresho halisi ya utendaji, uwajibikaji na utoaji wa huduma zenye viwango kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima nchini. Amesema mafanikio ya kupata cheti hicho yanapaswa kuwa msingi wa kujenga utamaduni wa ubora unaozingatia ufanisi, uwazi, uwajibikaji na maboresho endelevu, badala ya kukifanya kuwa nyaraka ya kutunzwa ofisini bila kuleta mabadiliko yanayoonekana katika huduma zinazotolewa. Dkt. Mwamba ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 kwa TIRA, iliyofanyika katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa kupata cheti hicho si mwisho wa safari ya ubora, bali ni mwanzo wa hatua mpya ya kuimarisha utendaji wa ...

JESHI LA MAGEREZA NA VETA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA URASIMISHAJI UJUZI KWA WAFUNGWA

  Na Ssgt Mawazo Mtondo - DODOMA. Mkuu wa Sehemu ya Viwanda wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Dkt. Uswege Mwakahesya, leo Novemba 18, 2026, ameongoza kikao cha maandalizi ya hafla ya kuwatunuku vyeti wafungwa 481 waliohitimu mafunzo ya ufundi kupitia Mfumo Usio Rasmi wa Mafunzo (RPL) chini ya Programu ya Mama Samia. Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Novemba 2026 katika Viwanja vya Gereza Karanga, mkoani Kilimanjaro, na itahusisha pia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Ushirikiano huo unalenga kutambua, kuthibitisha na kurasimisha ujuzi wa wafungwa ili kuwawezesha kutumia ujuzi huo kujiajiri au kuajiriwa wanaporejea katika jamii

DKT. MWIGULU: MSITWAE ARDHI ZA WANANCHI BILA FIDIA

  *_▪︎ Akemea matumizi mabaya ya mamlaka kuwatisha wamiliki wa maeneo_* *_▪︎ Ataka uwekezaji uwanufaishe pia wananchi wanaopisha miradi_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka maafisa wa ardhi kuzingatia sheria na kuhakikisha wananchi wanaopisha miradi ya maendeleo na uwekezaji wanalipwa fidia, akisisitiza kuwa matumizi ya maeneo hayo kwa manufaa ya umma hayapaswi kupuuza haki za wamiliki. Amesema katika maeneo mbalimbali amekutana na malalamiko ya wananchi ambao mashamba yao yametumika kujenga shule, vituo vya afya na kutekeleza miradi mingine, lakini hawajalipwa fidia licha ya huduma kuanza kutolewa. “Tuache kutumia vibaya sheria. Tuache kutumia vibaya mamlaka,” amesema. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mailimoja, Kibaha, mkoani Pwani, baada ya kuzindua kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa. Ameeleza kuwa Serikali inapohitaji ardhi kwa ajili ya miradi yenye maslahi mapana ya Taifa, wahusika wanapaswa kuzinga...