MBUNGE wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Waitara, amehoji mkakati wa Serikali katika kusimamia maadili kwa watumishi wa umma, akitaka kufahamu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na vitendo vya ushoga na usagaji ambavyo amedai vinaanzia katika shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali.
Akizungumza Novemba 4, 2026, Bungeni jijini Dodoma, Waitara amehoji namna Serikali inavyohakikisha watumishi wanaoingia katika ajira za umma wanazingatia maadili yanayokubalika katika jamii.
Akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amesema Serikali inaendelea kusisitiza umuhimu wa maadili kwa watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema Serikali pia imeimarisha elimu ya maadili kupitia mabadiliko ya mtaala wa elimu kwa kuanzisha somo la Historia na Maadili, linalolenga kuwajengea watoto uelewa wa maadili ya Kitanzania tangu wakiwa katika umri mdogo.

Comments
Post a Comment