📍Dodoma Tume ya Madini imesema kuanzishwa kwa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini nchini kumeongeza uwazi katika biashara ya madini na kusaidia kudhibiti utoroshaji wa rasilimali hiyo, hatua iliyochangia kuongezeka kwa mapato ya Serikali. Akizungumza leo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Afisa wa Tume ya Madini kutoka Kurugenzi ya Ukaguzi na Biashara ya Madini, Ibrahim Akyoo, amesema mfumo huo umewezesha wachimbaji na wafanyabiashara kuuza madini kupitia njia rasmi na hivyo kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo. Amesema kwa sasa nchini kuna masoko ya madini 44 na vituo vya ununuzi wa madini 120 vinavyorahisisha biashara ya madini na kuhakikisha Serikali inapata mapato stahiki yatokanayo na rasilimali hizo. Akyoo amesema miongoni mwa majukumu ya Kurugenzi ya Ukaguzi na Biashara ya Madini ni kusimamia biashara ya madini nchini, kuhakikisha ushiriki wa Watanzania katika sekta hiyo unaongezeka, kudhibiti ut...
Marato tv - Sauti ya Jamii