Wakizungumza kuhusu pambano hilo, wadhamini Cosmas Kenyata maarufu Bongo Jr na Wasonga Kenyata wa Bongo Jr wamesema kuwa maandalizi ya kuwapa wakazi wa Rorya burudani ya aina yake yanaendelea, huku wakiahidi siku hiyo kuwa ya kipekee kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi na wapenzi wa muziki.
Katika pambano hilo, bondia Mada Maugo, ambaye ni mmoja wa wana Rorya, atakutana na Mandonga Mtu Kazi katika mpambano unaotarajiwa kuongeza msisimko kwa mashabiki watakaofika kushuhudia makonde ya mabondia hao.
Mbali na pambano hilo la ngumi, mashabiki watapata fursa ya kufurahia burudani ya muziki kutoka kwa msanii Odongo Swaga kutoka nchini Kenya, jambo linalotarajiwa kuifanya siku hiyo kuwa ya burudani mseto kwa wakazi wa Rorya na maeneo jirani.
Mkurugenzi wa Bongo Jr ameamua kuwaletea wana Rorya burudani hiyo kwa namna tofauti, kwa kudhamini pambano hilo la ngumi na muziki ili kuwapa wakazi wa eneo hilo nafasi ya kufurahia Boxing Day kwa burudani ya kipekee.
Jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba kiingilio kitakuwa bure, hivyo wakazi wa Rorya na maeneo jirani wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Obwere, Shirati, Desemba 26, 2026, kushuhudia pambano hilo na kufurahia burudani ya muziki.
Kumekucha Rorya ya Moto, Hakuna Kulala! Ni Bongo Jr!





Comments
Post a Comment