Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi, jijini Mombasa, Kenya, leo tarehe 17 Juni 2026, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt. Mwinyi ameambatana na ujumbe wake, wakiwemo Mhe. Mama Mariam Mwinyi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe.
Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa uwanjani hapo na Waziri wa Michezo, Uchumi Ubunifu na Vijana wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Salim Mvurya Mgala, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mhe. Masoud Ali Mohamed, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Bernard Yohana Kibesse.
Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Mwinyi atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 11 wa Masuala ya Bahari (11th Our Ocean Conference).









Comments
Post a Comment