NA Mwandishi wetu Arusha ARUSHA Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Global Medicare inaendelea kuimarisha Hospitali ya JKCI-ALMC (Selian ya Mjini) Arusha kupitia uwekezaji wa miundombinu, teknolojia na vifaa tiba vya kisasa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya huduma za afya kuelekea mashindano ya AFCON 2027 na kuboresha huduma za kudumu kwa wananchi wa Kanda ya Kaskazini. Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Richard Kisenge, amesema maandalizi hayo yanahusisha uwekezaji mkubwa katika huduma za dharura, Sports Medicine, vifaa vya uchunguzi, teknolojia za ufuatiliaji wa wagonjwa pamoja na kuongeza uwezo wa hospitali kutoa huduma za kibingwa na kibobezi. Amesema ushirikiano na Global Medicare umechangia katika maboresho ya miundombinu na uwekezaji wa teknolojia za vifaa tiba, huku baadhi ya vifaa vipya vikiwa katika hatua mbalimbali za kuwasili na kufungwa katika JKCI-ALMC. “Tumeshirikiana na wenzetu wa Global Medicare katika kuhakikisha hospitali hii inaboresh...
Marato tv - Sauti ya Jamii