Akiwa jijini Dodoma, Rais Lourenço alishiriki hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba pamoja na miundombinu ya barabara zake.
Mheshimiwa Lourenço aliagwa rasmi na mwenyeji wake Rais Samia katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma kabla ya
kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
Katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma Mheshimiwa Lourenço alisindikizwa na kuagwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb.) Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.
Ngwaru Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.
Rosemary Senyamule, Balozi wa Tanzania anayewakilisha Angola mwenye makazi yake Zambia Injinia Cyprian Luhemeja, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Angola Bw.
Mbwana Mziray na viongozi wengine wa Serikali.






Comments
Post a Comment