Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.
Maboresho yaliyofanywa na Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) yapunguza muda wa ulipaji mafao kwa wanachama wake hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Katibu tawala mkoa wa Mara Gerald Musabila Kusaya amewaeleza wanachama wa NSSF wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja katika ukumbi wa ofisi za NSSF mkoani humo.
Kusaya amesema kuwa Maboresho hayo yameendelea kuongeza wigo wa ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wanachama na ulipaji wa mafao kwa wakati.
"Tunaona Maboresho yameendelea kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wanachama ya ulipaji wa mafao ambapo hivi sasa wastani wa muda wa kulipa mafao umepungua Kutoka siku 63 hadi kufikia siku 19 mafanikio haya ni makubwa matumizi ya mtandao yamerahisisha huduma kwa wateja", amesema Kusaya.
Juhudi hizi za serikali za kurahisisha huduma kwa wananchi wake ni uwajibikaji wa vitendo pia unaokoa muda wa huduma na kuwezesha kupatikana kwa wakati na jambo hili ni la dunia nzima huduma za kidijitali zinatumika kwa kiasi kikubwa ameongeza Kusaya.
Meneja wa NSSF mkoani Mara Emmanuel Kahensa amesema upatikanaji huduma bora umetokana na kuwasikiliza wateja mahitaji yao kuyatafakari na kuyafanyia kazi.
"NSSF inawahudumia wateja katika kila hatua na yanaonekana kwa vitendo na kuwezesha kusogeza huduma kiganjani na kufanya mageuzi makubwa waajiri,wanachama na wastaafu hupata huduma mbalimbali za NSSF kwa njia ya mtandao", amesema Kahensa.
Hivi sasa usajili, kufuatilia taarifa za michango kufungua na kufuatilia madai ya mafao na kufanya uhakiki wa wastaafu hakuhitaji kufika ofisi za mfuko hutumia huduza za kidijitali hivyo huwezesha kuokoa ghalama za nauli kwa mwanachama.
Aidha amefafanua kuwa ulipaji unazidi kushuka kutoka siku 19 hadi siku 5 hii inatokana na mfuko kuendelea kuboresha mifumo yake pia kutokana na sheria ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2018 mfuko umepewa jukumu la kusajili wananchi waliojiajiri na kuhakikisha wanawafikia wote kupitia hifadhi skimu.
Neema Bryson mwanachama wa NSSF kutokea Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma amesema amefurahishwa na elimu aliyoipata ambayo imemuwezesha kujiunga na sasa ananufaika na fao la matibabu.
Vile vile amewashauri wanawake wajasiriamali kujiunga kwa wingi kupunguza ghalama zisizo za lazima na kuhifadhi fedha na kujiletea Maendeleo na kukuza uchumi wao.
Gabriel Ogosi mkazi wa Tarime mkoani Mara amesema upatikanaji huduma kiganjani kumemsaidia hata akiwa shambani au malishoni anaweka michango yake bila tatizo lolote.
"Nimekuwa mwanachama wa NSSF muda mrefu miaka ya nyuma ilitulazimu kufika ofisi za mfuko kuweka michango na kujua taratibu zingine hivi sasa huduma zimeboreshwa zimekuwa za kidijitali ukiwa popote muda wowote unapata huduma bila changamoto yeyote", amesema Ogosi.
Amemalizia kwa kusema hii imewezesha uchumi wake kukuwa na kuwa na maendeleo makubwa katika kazi yake ya kilimo NSSF imebadili maisha yake kwa kiasi kikubwa amewahamasisha wakulima na wafugaji wajiunge kwa manufaa yao na familia zao.
Katika kilele hicho kiliambatana na utoaji wa vyeti na zawadi kwa wanachama wachangiaji bora wa hiari na kwa waajiri wanaowasilisha michango yao kwa wakati.
Wanachama waliopata vyeti vya uchangiaji bora ni pamoja na Gabriel Ogosi Mwing'a, Yohana Johanson Marwa,Elvis Samson Erick, Northmara field Group,Rhobi Nyakigendo,Enocy Daniel Meng'anyi,Juhudi Marwa Waryoba,Rukeke Rajabu Lusweka,Mariam Chacha na Rehema Majira Rajabu.
Waajiri waliopewa vyeti vya uwasilishaji michango kwa wakati ni North Mara Goldmine Limited,Fregom Limited Musoma,Grumet Reserves Limited,4c Protrade LTD, Beijing Construction Engineering Group Co LTD,Polygold Company Ltd,Grumet Construction Ltd,Mara mining Envestiment, CMS (Tanzania) Ltd,Grumet Air Ltd,The Registered Trusted of Grumet fund trust,Sisini Collection Ltd Serengeti,Henan Highway engineering Group, Company Ltd Musoma.
Pia na Asb Tanzania Ltd T/A Nogongoro, Member of Melia Collection,Taifa Mining&Civils Ltd (Tarime),Hero Rital Ltd Musoma,Buhemba Resources Ltd, na Sga Guards(T)Ltd Tarime.








Comments
Post a Comment