Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.
Ukuaji wa teknolojia unazidi kuimarisha huduma mbalimbali ambapo kwa kiasi kikubwa mifumo imekuwa sehemu ya kuwezesha maboresho ya huduma rahisi kwa wananchi.
Kwa umuhimu huo Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imehakikisha inaendelea kushiriki kikamilifu kuendana na mabadiliko ya teknolojia mkupunguza malalamiko kwa wananchi hasa katika huduma ya maji kwa kuja na njia mbadala ya matumizi ya teknolojia kwa kuleta mita za malipo kabla.
Hivi sasa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Musoma(MUWASA) kupitia Mkurugenzi Mtendaji Esther Gilyoma kwa kuhakikisha malalamiko yanapungua tayari mita za malipo kabla zimeanza kufungwa.
Gilyoma amesema ataendeleza ushirikiano na wananchi na yupo tayari kutoa na kupokea taarifa za huduma ya maji pamoja na uondoshaji wa maji taka.
Aidha katika mpango wa mwaka wa fedha wa 2026 mamlaka imejipanga kuwahudumia wananchi kwa kutumia teknolojia mpya na inaendelea kutii agizo la serikali ambapo Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda kuona wananchi hawalalamikii huduma ya maji.
"Tumekuwa tukishirikiana na wananchi kwa kutoa taarifa za mivujo,wizi wa maji na kupambana na upotevu wa maji,niendelee kuwahakikishia ushirikiano ulitukuka mimi Mkurugenzi na watendaji wenzangu hatutakuwa kikwazo tupo hapa kwa kuwahudumia wakati wote ushirikiano huu uendelee,"amesema Gilyoma.
Ameongeza kuwa maendeleo ni hatua MUWASA inaendea kusambaza mita za malipo baada na za Malipo kabla mita zote zimehakikiwa na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA).
" MUWASA tayari imeleta mita za malipo kabla zipatazo 500 na zimeanza kufungwa kwa wateja lengo ni kuondoa malalamiko kwa wateja na mamlaka inaendelea kujipanga na kuhakikisha teknolojia hiyo inawafikia wengi na waendelee ".
Ifahamike kuwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanzania (WSSAs)ni mashirika ya serikali yanayosimamia uzalishaji,usambazaji wa maji safi, na usimamizi wa majitaka hufanya kazi chini ya uangalizi wa Wizara ya Maji na kudhibitiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)huku Idara ya Maji ikihusika na usimamizi, uendelezaji na upatikanaji wa rasilimali za maji na huduma za majisafi.
Malipo ya huduma ya maji hutozwa kulingana na matumizi ya mteja ambapo mita ya ujazo hutozwa kwa kiwango kilichopangwa na EWURA ujazo kuanzia 1-5 ghalama zipo chini kuanzia 6 na kuendele malipo yake huongezeka.
Gilyoma amewakumbisha na kuwahimiza wateja kufuatilia taarifa za usomaji mita ili kama kuna changamoto iwasilishwe MUWASA kwa kutatuliwa usomaji mita huambatana na ujumbe anaoupata mteja kupitia namba yake ya simu na kufahamu mita za ujazo alizotumia.



Comments
Post a Comment