Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo Manyinyi ashiriki mazishi ya Benadetha Joseph Marwa mama mzazi wa George Marato aliyefariki Oktoba 9,2026 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa maradhi ya moyo.
Maziko yamefanyika Oktoba 14,2026 kijiji cha Ryamisanga wilayani Butiama mkoani Mara na kuhudhuliwa na waombolezaji kutoka mikoa mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali na wa vyama vya siasa.
Ibada ya Mazishi imefanyika katika Parokia ya St, Augustine iliyopo Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma iliyoongozwa na Paroko John Chacha.
Marehemu Benadetha Joseph Marwa ni muumini wa Parokia hiyo pia ni mwanajumuiya ya Mtakatifu Roza wa Lima.
Mara baada ya mazishi viongozi na baadhi ya waombolezaji walipata fursa ya kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya George Marato.
Akitoa salamu za rambirambi Vedastus Mathayo amewasisitiza kuendeleza mshikamano walionao huku akiwapa moyo katika kipindi hiki cha majonzi.
"Mshikamano mlionao tangu wakati wa maradhi hadi kumpumzisha Benadetha katika nyumba yake ya milele muuendeleze siku zote", amesema Mathayo.
Viongozi waliohidhulia mazishi hayo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Butiama Christopher Marwa Siagi akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM mkoa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Mara Mfalme Julius Masubo Kambarage,Profesa Francis Chacha, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Butiama Michael Makenji,Mkuu wa Wilaya mstaafu Ibrahim Marwa.
Viongozi wengine ni Madiwani wa Manispaa ya Musoma wakiongozwa na Meya Alex Nyambiti naibu Meya Haji Mtete,wajumbe wa kutoka chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa,na baadhi ya waandishi wa habari wakiongozwa na Kaimu katibu wa klabu ya waandishi wa habari Mara (MRPC)Fresha Kinasa.
Kamati ya mazishi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi Marwa Masagati,majirani kutoka jijini Dar es Salaam, Musoma,na Ryamisanga.
Aidha Familia imewashukuru madaktari na wauguzi wote, viongozi wa vyama na serikali, viongozi wa dini,wanamusoma,ndugu,jamaa na marafiki,wadau mbalimbali,vyombo vya usalama,vikundi na taasisi mbalimbali na wote kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi hiki cha majonzi.














Comments
Post a Comment