Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
MATUMIZI ya dawa za kulevya bado ni changamoto kwa jamii, licha ya juhudi za serikali kwa kushirikiana na taasisi pamoja na mashirika yaisiyo ya kiserikali kupiga vita matumizi hayo na kuendelea kutoa elimu.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kinga dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwa wadau mbalimbali wakiwemo wahudumu wa afya ,maafisa maendeleo ya jamii,walimu na vijana Naibu Meya wa Jiji la Tanga Khalid Rashid amesema jiji limejipanga vizuri kukabiliana na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya kwa kuimarisha utoaji wa elimu na kushirikiana na wadau muhimu kuwalinda vijana dhidi ya madhara yatokanayo na dawa hizo.
Aidha Khalid ameongeza kuwa Tanga kupakana na nchi jirani imekuwa ikiathiri sana jiji hilo kwani madawa mengi yamekuwa yakiingizwa kutoka nje na hayatengenezwi Tanga,hivyo basi amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kumaliza tatizo hilo kwani jiji peke yao hawawezi.
"Tatizo la madawa hatutengenezi sisi yanatoka nje,na Tanga tumepakana na nchi jirani ya Kenya nayo ni sehemu kubwa inayotiathiri na pia tupo mwambao wa bahari ambapo kitafiti inaonesha pia hutumika kama njia ya kuingiza dawa hizo za kulevya,pia
tunashirikiana sana na jamii kwani waathirika wakubwa ni wanajamii na hili jambo linatuumiza sana sisi kama viongozi", amesema Khalid.
Nae Katibu Mtendaji wa shirika la Gift of Hope Said Bandawe amesema washiriki wapatao 22 kupatiwa mafunzo ya kinga ya dawa za kulevya kwa muda wa siku tano na baada ya hapo nao kuwa wakufunzi na kwenda kueneza elimu hiyo katika maeneo yao.
Aidha Bandawe ameongeza kuwa mafunzo hayo yametolewa kupitia mradi wa "Focus on Youth,Not Substance" "Tuzingatie Vijana,Na sio Dawa za Kulevya" unaolenga kzuia unyapaa na ubaguzi dhidi ua vijana wanaotumia dawa za kulevya ,kupunguza madhara na ukarabati wa vijana walio hatarini,kupunguza hatari ya matumizi ya dawa za kulevya kupitia ushirikishwaji wa jamii,elimu na kampeni za uhamasishaji.
Pia mafunzo hayo yanaendeshwa kwa kushirikiana na programe ya Tanga Yetu inayofadhiliwa na Foundation Botnar na kutkelezwa na innovex kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga,ikiifanya Tanga kuwa Jiji ambalo vijana wanastawi.



Comments
Post a Comment