Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MAOFISA 39 WA JESHI LA MAGEREZA WAPANDISHWA VYEO

Na. Wdrs Irine Nkana - DODOMA ‎Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP), Jeremiah Yoram Katungu, leo Oktoba 19, 2026, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, amewavalisha vyeo Maafisa 39 wa Jeshi la Magereza, wakiwemo Naibu Makamishna 17 na Makamishna Wasaidizi Waandamizi 22, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Msalato, jijini Dodoma. ‎Akizungumza katika hafla hiyo, CGP Katungu amemshukuru Rais kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza kwa kujaza nafasi za uongozi, kuboresha stahiki za watumishi na kutoa vibali vya ajira. Amesema kupandishwa vyeo kwa idadi hiyo ya Maafisa ni tukio la kihistoria, huku akiahidi kuwa Jeshi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi. ‎Amewataka Maafisa hao kutumia vyeo walivyopata kuongeza bidii na kusimamia majukumu ya Jeshi, ikiwemo kutoa hifadhi salama kwa wafungwa na mahabusu, kutekeleza programu za urekebu na kutoa ushauri wa kuzuia uhalifu katika jamii. ‎Kwa upande wake, Kamishna wa Sh...

WAWEKEZAJI WATAKIWA KUCHANGIA FURSA ZILIZOPO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ina ardhi kubwa na yenye retuba ya kutossha inayofaa kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kuifanya wilaya hiyo kuwa na fursa nyingi za uwekezaji katika kilimo na biashara. Hayo yameelezea na Mkurungenzi wa Halmashauri ya hiyo Naima Chondo kufuatia ushindi wa kitaifa  waliopata katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya usagara jijini Tanga. Hivyo basi Chondo amewakaribisha wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo katika halmashauri hiyo ikiwemo katika sekta ya Kilimo kwa kuwekeza katika uzalishaji wa mazao ya kisasa na kujenga viwanda vya kuchakata mazao hayo ili kuongeza thamani na kipato kwa wakulima. Chondo ameendelea kusema kuwa maandalizi mazuri na juhudi za kuwawezesha wakulima wadogo kushiriki maonesho ya siku ya chakula duniania pamoja na  kujifunza teknolojia mpya za kilimo na kupata fursa ya kuonesha ubora wa mazao wanayozalisha na mnyororo mzima wa thamani...

ASKARI WANAFUNZI 1,561 WA JESHI LA MAGEREZA WAHITIMU MAFUNZO YA AWALI KIWIRA

Na Ssgt Mawazo Mtondo - MBEYA. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, leo Oktoba 17, 2026, amefunga rasmi mafunzo ya awali ya Askari Wanafunzi wa Jeshi la Magereza, Kozi Na. 33, yaliyodumu kwa takribani miezi tisa katika Chuo cha Magereza Kiwira, jijini Mbeya. Jumla ya askari wanafunzi 1,561 wamehitimu mafunzo hayo, wakiwemo wanawake 367 na wanaume 1,194, kati ya wanafunzi 1,564 walioanza mafunzo. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Rwezimula amewataka wahitimu kutekeleza majukumu yao kwa bidii, uadilifu na nidhamu, kwa kuzingatia sheria na taratibu za Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla, huku wakitanguliza maslahi ya Jeshi na Taifa. Pia, amewasisitiza kuzingatia tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa hali ya hewa kuhusu mvua za El Nino. Baada ya kukagua gwaride la wahitimu, Dkt. Rwezimula alizindua nyumba tatu za makazi ya askari zenye uwezo wa kuhudumia familia sita. Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Magereza amemshukuru Rais wa Jamhu...

TCB YAJA NA MFUMO WA USHINDANI KATIKA UNUNUZI WA PAMBA MSIMU WA 2026/2027

 BODI ya Pamba Tanzania (TCB) imeweka mikakati ya kuimarisha ushindani katika ununuzi wa pamba msimu wa 2026/2027, sambamba na kuimarisha uwazi kupitia mifumo ya kidijitali katika usambazaji wa pembejeo na matumizi ya mizani janja ili kulinda maslahi ya wakulima. Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Mhandisi Godwin Makori, amesema katika msimu huo hakutakuwa na mnunuzi mmoja pekee katika kituo cha ununuzi wa pamba, hatua inayolenga kuongeza ushindani na kuwapa wakulima fursa ya kupata bei nzuri ya zao hilo. Amesema mfumo huo unatarajiwa kuwapa wanunuzi fursa ya kushindana, huku wakulima wakinufaika na uwezekano wa kupata bei inayolingana na thamani ya mazao yao.  Hatua hiyo inalenga kuongeza kipato cha wakulima na kuimarisha uchumi wa kaya zinazotegemea kilimo cha pamba. Katika hatua nyingine, TCB inatarajia kusambaza tani 15,000 za mbegu za pamba katika wilaya 56 zinazolima zao hilo nchini katika msimu wa 2026/2027.  Hadi wakati wa...