Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ina ardhi kubwa na yenye retuba ya kutossha inayofaa kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kuifanya wilaya hiyo kuwa na fursa nyingi za uwekezaji katika kilimo na biashara.
Hayo yameelezea na Mkurungenzi wa Halmashauri ya hiyo Naima Chondo kufuatia ushindi wa kitaifa waliopata katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya usagara jijini Tanga.
Hivyo basi Chondo amewakaribisha wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo katika halmashauri hiyo ikiwemo katika sekta ya Kilimo kwa kuwekeza katika uzalishaji wa mazao ya kisasa na kujenga viwanda vya kuchakata mazao hayo ili kuongeza thamani na kipato kwa wakulima.
Chondo ameendelea kusema kuwa maandalizi mazuri na juhudi za kuwawezesha wakulima wadogo kushiriki maonesho ya siku ya chakula duniania pamoja na kujifunza teknolojia mpya za kilimo na kupata fursa ya kuonesha ubora wa mazao wanayozalisha na mnyororo mzima wa thamani kuanzia shambani hadi sokoni ndio chachu ya ushindi huo kwao.
Kwa upande wake mkulima kutoka wilaya ya Muheza katika kata ya Amani Dastan Dafa ameishukuru serikali kwa kuwapatia fursa kama hizi ambazo hulenga kuwaongezea ujuzi na maarifa kwani hata baada ya maonesho haya amekiri kujifunza mbinu zitakazo muwezesha kuongeza tija na thamani ya bidhaa zao.
Dafa Amezitaja baadhi ya fursa zilizopo kuwa ni kilimo cha mahindi, ndizi na mazao ya viungo kama karafuu, iliki na mdalasini, ambayo yanaweza kunufaisha wakulima na wafanyabiashara kupitia masoko ya ndani na nje ya nchi.





Comments
Post a Comment