Na Mwandishi Wetu Jarida la _Forbes Africa_ limetaja Kampuni ya Kitanzania, Dar es Salaam Merchant Group - DMG, kama kampuni bora ya daraja la kwanza “Class One” katika eneo la ujenzi na ukarabati wa meli nchini Tanzania. Jarida hilo maarufu Afrika na duniani limeitaja DMG mara baada ya ufanisi mkubwa kwenye ukarabati unaoendelea wa Meli ya MV Liemba - meli kongwe zaidi duniani inayobeba abiria, iliyotengenezwa na Wajerumani zaidi ya miaka 110 iliyopita. _Forbes Africa_ imeielezea DMG kuwa inatengeneza na kukarabati meli kwa kutumia teknolojia ya kisasa, huku ikizingatia viwango vya juu vya usalama na utendaji. Katika kurasa 20-21 za toleo la Juni/Julai 2026 “Africa’s New Blueprint for Growth: Tanzania”, jarida hilo limesema DMG imeifanya Tanzania kuwa mojawapo ya nchi mbili pekee barani Afrika zenye uwezo wa kutengeneza na kukarabati meli kwa kiwango cha daraja la kwanza. Makala hiyo yenye kichwa _“Uwezo wa Tanzania wa Ujenzi wa Meli Daraja la Kwanza”_ inaeleza jinsi DMG, k...
Marato tv - Sauti ya Jamii