Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali vya michezo nchini ili viweze kutumika katika michuano ya kimataifa hata baada ya Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027). Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, mara baada ya kutembelea na kukagua usimikaji wa Viti katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga leo Juni 5, 2026. Mhe. Mwinjuma ameupongeza Uongozi wa uwanja huo chini ya Meneja Nassoro Makau, kwa kufanya ubunifu mkubwa wa kuvipanga vizuri viti kwa rangi, ikiwa ni viti vilivyotolewa na Serikali katika uwanja wa Benjamin Mkapa, hatua inayoupendezesha uwanja huo wa kihistoria. Amesema, uboreshaji wa viwanja vya michezo nchini ni sehemu ya maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye Serikali yake ya Awamu ya Sita imewekeza kwa kiwango cha hali ya juu katika ukarabati wa viwanja kama Uhuru na Mkapa, pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa Arusha. "Zoezi la usimikaji wa viti hapa Mkwakw...
Marato tv - Sauti ya Jamii