Tarehe 21 Oktoba 2026, Dar es Salaam.
Benki ya Azania imezindua kampeni ya PIGA NDEEFU, inayolenga kuhamasisha Watanzania kuweka akiba huku ikiimarisha uwezo wa Benki kufadhili biashara katika sekta mbalimbali kuelekea mashindano ya AFCON 2027 yatakayofanyika Tanzania, Kenya na Uganda.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Ndg. Samson Mahimbi, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa na Biashara za Kiserikali, amesema kampeni hiyo inalenga kukuza utamaduni wa kuweka akiba na kuchochea shughuli za kiuchumi, hususan katika sekta za utalii, malazi, usafiri na huduma nyingine zitakazowanufaisha wageni na mashabiki wa AFCON 2027.
Kupitia PIGA NDEEFU, wateja wanaweza kuanza kuweka akiba kwa TZS 500,000, kupata riba ya hadi 12% kwa mwaka na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo tiketi za mechi za ufunguzi na fainali za AFCON 2027, simu janja, televisheni na fedha taslimu, kwa kuzingatia vigezo na masharti ya kampeni.
Kampeni hii itaendelea hadi tarehe 21 Julai 2027.








Comments
Post a Comment