Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MKAKATI WA MAZINGIRA WAWEKWA MAENEO YENYE UCHAFU KUPEWA KINYAGO CHA FISI MANISPAA YA MUSOMA.


 Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.

Manispaa ya Musoma mkoani Mara yaweka mkakati kukabiliana na uchafu wa mazingira maeneo yaliyo machafu kukabidhiwa kinyago cha fisi.

Utaratibu huo umewekwa na Ofisi ya mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo wakiwemo viongozi wa Kata.

October 7,2026 utoaji wa tuzo za usafi na vinyago vya fisi vimetolewa kwa makundi mbalimbali kutoka kata, mitaa na shule.

Uondoshaji taka huu unafanyika katika kata zote 16 zilizopo katika Manispaa hiyo kwenye barabara, Kaya,maduka,masoko,stendi za mabasi, taasisi viwanja vya michezo na maeneo ya wazi.

Katika hafla hiyo ya utoaji tuzo hizo zimehudhuriwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka ambapo amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na litakuwa linafanyika kila mwezi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na kuweka usalama wa afya za wananchi.

"Usafi unapaswa kuwa miongoni mwa vipaumbele na kila mmoja anatakiwa kuwajibika kuweka mazingira safi kuanzia mashuleni,majumbani,mitaani na kwenye maeneo yote hapa Musoma", amesema Chikoka.

Ameongeza kuwa matarajio ni kuufanya mji wa Musoma kurudi kuwa kinara wa usafi kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma na kwa kulifanikisha hilo tayari mpango wa uwekaji mapipa ya kuhifadhia taka utaanza wiki ijayo lengo likiwa kuwezesha wananchi kuwa na maeneo rasmi ya kuweka taka.

Kwa mujibu wa mkuu wa Idara ya usafi wa mazingira Mwizarubi Nyahindi amesema kiasi cha taka zinazozalishwa kwa mwaka katika manispaa ni tani 32 katika kiwango hiki zinazokusanywa ni tani 19.2 na zinazolejerezwa ni tani 6 na taka zinazozalishwa ni zinazooza,vifingashio(makopo na karatasi) na vioo(Chupa za glass).


Amefafanua hali ya miundombinu ya ukusanyaji taka iliyopo kuwa kuna eneo la dampo lenye ekkari 25,ghuba moja soko la kwa saa nane,vitunzia taka(dustbin)12,mkokoteni1 na magari ya kubebea taka 2.

Ukusanyaji taka huo unahudumiwa na wazabuni ambao wanahudumia Kata tisa ambao ni Jeshi la Magereza ambao wanahudumia Kata nne za mjini,Musoma Cleaners,Cathel,Kikundi cha usafi Nyakato,Kikundi cha usafi mshikamano,Chide securities and cleaning services na Elimat general services Limited.

Aidha Mwizarubi hakusita kuelezea changamoto iliyopo ya upungufu wa maafisa afya ambapo kwa sasa kuna maafisa afya 6 pekee hali inayopelekea kuwepo kwa changamoto katika usimamizi wa usafi.

Amesema hivi sasa tayari mikakati ya kuomba kibali cha kuajiri maafisa afya wa kutosheleza umefanyika hivyo ni mategemeo ya kuhakikisha usimamizi wa usafi unaboreshwa.

Nae Mihayo Pastory Mnyeti afisa elimu Kata ya Nyakato ambae ni miongoni mwa waliopata tuzo na kuwa kinara wa usafi kwa Shule za msingi amepongeza hamasa hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa safi.

Amehisihi na kuwapa moyo waliopata tuzo ya vinyago vya fisi kutojihisi wanyonge bali waongeze bidii ya uimalishaji na usimamizi wa usafi wa mazingira katika maeneo yao.

Hata hivyo afisa afya Chacha Mugesi amewasihi wananchi wote kuacha tabia ya utupaji taka hovyo kwa kuwa taka husababisha magonjwa mbalimbali ya mlipuko yanayopelekea kuhatarisha afya zao.

Usafi ni muhimu kwa afya njema na huepusha maradhi ya mlipuko yanayoweza kusababisha hata vifo ni muhimu kuzingatia usafi wa mazingira kwa kuwa uchafu ni chanzo maradhi yanayoepukika mazingira ni uhai kwa viumbe hai.

Miongoni mwa waliopata tuzo ya fisi ni mtaa wa Makoko ziwani, Shule ya msingi Nyasho A, sekondari ya Bweri huku washindi wakiwa waliopata tuzo ni pamoja na mtaa wa Mwigobero D na B,Kitaji A na Kata zilizofanya vizuri ni pamoja na Kata ya Mwigobero,Kitaji na Mwisenge na tuzo hizi zitatolewa kila mwezi kwa mujibu wa mkuu wa Wilaya ya Musoma.






Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...