Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. MSEMO: SARATANI INATIBIKA, HASA INAPOGUNDULIKA MAPEMA

 



WANANCHI wametakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara na kutafuta huduma za kitabibu mapema, kwa kuwa saratani inaweza kutibiwa kwa ufanisi zaidi inapogundulika katika hatua za awali.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dkt. Diwani Msemo, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, Agosti 19, 2026, jijini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa wananchi kuondokana na dhana potofu kuhusu saratani na kuchukua hatua za mapema katika afya zao.


Dkt. Msemo amesema wananchi wanapaswa kufahamu kuwa saratani si ugonjwa usiotibika, hasa pale inapogundulika mapema, huku akiviomba vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na ORCI kutoa elimu sahihi kwa umma kuhusu kinga, uchunguzi na matibabu ya saratani.


Katika hatua nyingine, Serikali imeongeza uwekezaji mkubwa katika huduma za saratani kupitia ORCI, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza uwezo wa uchunguzi na matibabu, kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri huduma na kuimarisha nafasi ya Tanzania kuwa kituo muhimu cha huduma za saratani katika Afrika Mashariki na Kati.


Dkt. Msemo amesema uwekezaji huo unaenda sambamba na ujenzi wa vituo vipya, ununuzi na ufungaji wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba, ukarabati wa miundombinu, pamoja na kuimarisha rasilimali watu na mifumo ya TEHAMA.


Amesema miongoni mwa miradi mikubwa ni ujenzi wa Kituo cha Saratani Mbeya, wenye thamani ya Sh bilioni 11, ambao umefikia takribani asilimia 57 na unatarajiwa kukamilika Januari 2027, huku huduma zikitarajiwa kuanza Julai mwaka huo.


Kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia wananchi wa Mbeya na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, pamoja na wagonjwa kutoka nchi jirani za Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Aidha, ORCI inaendelea na ujenzi wa Multipurpose Oncology Building jijini Dar es Salaam wenye thamani ya takribani Sh bilioni 5.9. Mradi huo umefikia asilimia 65 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2026.

Kwa mujibu wa Dkt. Msemo, jengo hilo litakuwa na wodi, maeneo ya tiba ya kemikali, kliniki za saratani, maabara, famasia na ofisi za wataalamu, hatua inayolenga kupunguza msongamano na kuboresha mazingira ya wagonjwa.


Katika tiba ya mionzi, amesema ORCI imekamilisha mradi wa Linear Accelerator wenye uwekezaji wa takribani Sh bilioni 7.9, ukiwemo ujenzi na ukarabati wa chumba maalumu pamoja na ununuzi na usimikaji wa mashine hiyo.


Amesema mashine hiyo tayari imeanza kutoa huduma na inalenga kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri kuanza matibabu hadi wastani wa takribani wiki mbili.


ORCI pia imeagiza mashine mbili za Cobalt kwa ajili ya tiba ya mionzi zenye thamani ya takribani Sh bilioni 4, huku ukarabati wa vyumba maalumu ukigharimu Sh milioni 300. Usimikaji wa mashine hizo umefikia asilimia 95 na zinatarajiwa kuanza kutumika Septemba 2026.


Kwa upande wa uchunguzi wa saratani ya matiti, Dkt. Msemo amesema ORCI imenunua mashine mbili mpya za Mammography zenye thamani ya takribani Sh bilioni 1.1. Mashine hizo zimewasili nchini na usimikaji unaendelea.

Aidha, amesema ORCI inaendelea na ufungaji wa PET Scan yenye thamani ya Sh bilioni 18.2, teknolojia inayosaidia kuonesha shughuli za viungo vya mwili, kugundua saratani na kufuatilia iwapo imeenea katika maeneo mengine ya mwili.


Amesema uwepo wa teknolojia hiyo utaongeza uwezo wa Tanzania katika uchunguzi na ufuatiliaji wa saratani na kuimarisha nafasi ya nchi katika utoaji wa huduma za kisasa za saratani barani Afrika.


Dkt. Msemo amesema taasisi hiyo pia imefunga mashine ya kisasa ya tiba ya mionzi aina ya ELEKTA Harmony, yenye thamani ya Sh bilioni 8.3, inayotumia teknolojia ya Image Guided Radiotherapy (IGRT) kusaidia kulenga eneo lenye uvimbe kwa usahihi zaidi huku ikilinda tishu na viungo vilivyo karibu.


Mashine nyingine ni SPECT, yenye thamani ya Sh bilioni 1.5, inayotumia teknolojia ya mionzi maalumu kusaidia kuonesha namna viungo vya mwili vinavyofanya kazi.


Mbali na uwekezaji katika teknolojia, amesema ORCI imeendelea kuimarisha maabara, rasilimali watu na mifumo ya TEHAMA kwa lengo la kuboresha usimamizi wa taarifa za wagonjwa na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.


Amesema taasisi hiyo pia imeimarisha huduma za uchunguzi wa mapema na kinga kupitia kampeni ya Tiba Mkoba, ambayo tayari imefika katika mikoa 15 na kuwafikia zaidi ya watu 200,000 kwa huduma za uchunguzi wa awali wa saratani.


Katika hatua nyingine, Dkt. Msemo amesema ORCI inatarajia kuanza kutoa huduma za upasuaji mkubwa wa saratani Oktoba 2026 baada ya kukamilika kwa vyumba vya upasuaji.

Amesema madaktari bingwa saba wa upasuaji tayari wamerejea nchini baada ya mafunzo, huku wataalamu wengine wanne wakiendelea na masomo.


Kwa mujibu wa Dkt. Msemo, upanuzi huo wa huduma unalenga kuifanya ORCI kuwa kituo kinachoweza kutoa huduma pana za kibingwa za saratani na kupunguza utegemezi wa wagonjwa kusafiri nje ya nchi kwa baadhi ya huduma.


Aidha, ORCI inaandaa mipango ya kuanzisha vituo vipya vya saratani katika mikoa ya Mtwara, Kigoma na Arusha, huku ikiendelea na maandalizi ya kuanzisha ORCI Consultancy Bureau, itakayotoa utaalamu katika ununuzi, usimikaji, matengenezo na matumizi ya vifaa tiba.


Dkt. Msemo amesema ORCI pia imeweka mpango wa kuwezesha uzalishaji wa dawa na bidhaa zinazotumika katika matibabu ya saratani nchini, hatua inayolenga kupunguza utegemezi wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.


Amesisitiza kuwa uwekezaji huo unalenga kuimarisha huduma za kinga, uchunguzi, tiba, utafiti na mafunzo ya saratani, huku ukifungua fursa ya Tanzania kuwa kituo cha rufaa kwa wagonjwa kutoka ndani na nje ya nchi.


Hata hivyo, Dkt. Msemo amesisitiza kuwa pamoja na uwekezaji huo, hatua muhimu zaidi inaanzia kwa wananchi wenyewe—kupima afya mara kwa mara, kutambua dalili mapema na kufika hospitalini kwa wakati.


Amesema ushirikiano kati ya wananchi, wataalamu wa afya na vyombo vya habari ni muhimu katika kuongeza uelewa wa jamii na kupunguza hofu pamoja na dhana potofu kuhusu saratani.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...