Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) kuwasaidia wabunifu kuweza kufikia malengo yao,kuwezesha watu kupata ajira kupitia bunifu na kusaidia taifa kupata teknolojia mpya kupitia mashindano ya ubunifu na teknolojia.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa tume hiyo Prof. John Kondoro alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari siku ya uzinduzi wa maonesho ya wiki ya elimu ujuzi na ubunifu .
Prof. Kondoro amesema kuwa mashindano ya ujuzi na ubunifu yanafaida kubwa katika kuhamasisha na kuendeleza bunifu mpya nchini sambamba na kuwezesha bunifu mbalimbali.
Ilikufanikisha hayo yote Prof. Kondoro amesema COSTECH haifanyi kazi peke yake bali hushirikiana na taasisi nyingine zinazohusika na utafiti,ubunifu na teknolojia kama vile taasisi ya elimu ya juu,VETA, DIT na nyinginezo ili kuwasaidia wabunifu kukuza na kuendeleza mawazo yao.
COSTECH pia Ina mfuko Kwa ajili ya kuwawezesha kifedha wabunifu ili kuweza kufika sokoni kwani waliowengi hushindwa kutimiza malengo Yao kutokana changamoto za mitaji.



Comments
Post a Comment