Agosti 18, 2026. Mbunge wa Jimbo la Uyole na Rais wa IPU Mhe. Dkt. Tulia Ackson ametembelea na kukagua miundombinu ya shule ya msingi Iganjo kata ya Igawilo Jimbo la Uyole na kuangalia hali ya wanafunzi ambapo ametoa ahadi ya kuiomba serikali kuweza kusaidia kuboresha miundombinu ya shule hiyo pamoja na kuongezwa kwa matundu ya vyoo katika shule hiyo.
Wakati huohuo Dkt. Tulia ametoa ahadi kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuchangia kompyuta, mashine ya kutolea nakala (printer mashine) hivi karibuni ili kuweza kurahisisha shughuli za elimu katika shule hiyo.






Comments
Post a Comment