Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TANZANIA YAJIPANGA KUWA MZALISHAJI MKUBWA WA MADINI KINYWE(GRAPHITE)DUNIANI


■ Sera imara na usimamizi thabiti wa Mhe. Rais Samia kuchochea uzalishaji

■ Serikali yasaini mkataba wa ubia wa uchimbaji wa madini kinywe na Kampuni ya Lindi Jumbo

■ Tani 40,000 kuzalishwa kwa mwaka, kwa zaidi ya miaka 24.

▪️Waziri Mavunde awataka wamiliki wa Leseni 28 za uchimbaji wa madini kinywe kuanza uzalishaji kabla hawajafutiwa Leseni


*Ruangwa, Lindi*

Waziri wa Madini, *Mh. Anthony Mavunde (Mb)* amesema kwamba Tanzania inajiapanga kuwa mmoja ya wazalishaji wakubwa Duniani wa madini kinywe(𝙂𝙧𝙖𝙥𝙝𝙞𝙩𝙚) kupitia Kampuni 30 zinazomiliki Leseni za kati na kubwa za uchimbaji wa madini hayo na hivyo kutoa ushindani wa kiuzalishaji kwa nchi ya China ambayo ndio inaongoza kwa uzalishaji wa madini hayo duniani kwa kuzalisha tani milioni 1.2 kwa mwaka. 

Mh. Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 28 Mei, 2026 Wilayani Ruangwa, Lindi aliposhiriki katika hafla ya utiaji saini wa mikataba wa ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Lindi Jumbo Limited kwa ajili ya mradi mkubwa wa uchimbaji madini kinywe na kubainisha kuwa kuanza kwa uchimbaji mkubwa wa madini mkakati ya kinywe (graphite) kunaiweka Tanzania kwenye dira ya duniani kama Nchi ya kimkakati katika uzalishaji wa madini hayo muhimu kwenye utengenezaji wa betri za magari ya umeme.



"Mhe. Rais *Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kuijenga na kuifanya Nchi yetu ya Tanzania kama Taifa lenye dira wazi ya kiuchumi, mazingira rafiki ya uwekezaji na usimamizi imara wa rasilimali zake"

"Tukio la leo ni matokeo ya dira na maono hayo thabiti ya Mhe Rais ambayo yameendelea kuifanya Tanzania kuwa sehemu salama ya wawekezaji ambayo ina sera na Sheria zinazoeleweka na kutabirika" alisisitiza Mhe. Mavunde. 

Mhe. Mavunde amefafanua pia kwamba kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya sita Duniani kwa uzalishaji wa madini kinywe ambapo kwa mwaka uzalishaji wa Tanzania ni tani 25,000 kwa kampuni mbili tu zilizoanza uzalishaji mkubwa za Lindi Jumbo na God Mwanga-Tanga huku zingine 28 zikiwa katika hatua mbalimbali za kuanza uzalishaji.

Mh. Mavunde amewataja wamiliki wa Leseni 28 za uchimbaji madini kinywe kuhakikisha wanaanza uzalishaji mapema kama sheria inavyoelekeza ili kuepuka kufutuwa leseni hizo.

Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa dunia kwa sasa inapita kwenye mageuzi makubwa ambapo madini kinywe ni msingi wa kesho kwani upatikanaji wake ni kichocheo kikubwa katika uzalishaji wa nishati safi kwa kusaidia utengenezaji betri za magari ya umeme.

Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 82 unataraji kuzalisha madini kinywe tani 40,000 kwa mwaka katika kipindi cha uhai miaka 24 ya mgodi ambapo zaidi ya ajira 300 zimezalishwa hadi sasa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Timu ya Majadiliano ya Serikali kwenye sekta ya madini, *Prof. Sifuni Mchome* alieleza kuwa miongoni mwa faida ambazo Serikali itapata kupitia kusaini mikataba hiyo ya ubia ni pamoja na udhibiti wa fedha na uhakika wa mapato kutokana na uwekezaji huo na fursa za ajira kwa watanzania.

Prof. Mchome alibainisha kuwa kupitia makubaliano hayo yaliyotiwa saini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itamiliki asilimia 16 ya hisa huru zisizohafifishwa thamani (non-dilutable free carried interest shares), huku Kampuni ya Lindi Jumbo Limited ikimiliki asilimia 84 ya hisa katika kampuni ya ubia.

Awali, akieleza maendeleo ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Lindi Jumbo Limited, *Bw. Andrew Cunningham* alibainisha kuwa pamoja na upanuzi wa uzalishaji wa mgodi huo, wataendelea kufanya utafiti ili kubaini mashapo zaidi ambayo yatarefusha maisha ya mgodi na kuongeza manufaa zaidi kwenye uchumi wa Tanzania.


Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, *Mheshimiwa Mohamed Moyo* aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuvutia wawekezaji ambayo wamekuwa ni chachu ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi na kuahidi kwamba Serikali ya Mkoa wa Lindi itaendelea kuwapa ushirikiano wawekezaji wote ili wafikie malengo yao na kuchochea uchumi wa Nchi yetu.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...