Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Hati ya Makubaliano ya Kuandaa Afcon 2027 Yasainiwa

Nchi waandaji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027) wamesaini hati ya makubaliano ya pamoja inayojulikana kama CAF Joint Resolution – TotalEnergies AFCON PAMOJA 2027 tarehe 11 Mei, 2026. Nchi hizo ambazo ni Tanzania Kenya na Uganda zimesaini hati hiyo kwa lengo la kuimarisha uratibu na ushirikiano katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika. Utiaji saini makubaliano hayo yameshuhudiwa na  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motssepe.  Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais Wallace Karia. 

Dkt. Lyembe Aipongeza Bajeti ya Wizara ya Afya, Tabora Kuanza Huduma za Kusafisha Figo

MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete), Dkt. Joachim Lyembe ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuwasilisha bajeti aliyoieleza kuwa ni ya kimkakati katika kuboresha huduma za afya nchini, hususan mpango wa ujenzi wa hospitali mpya ya Taifa Muhimbili. Dkt. Lyembe amesema maboresho hayo yanaakisi dhamira ya Serikali ya Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha sekta ya afya na kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi. “Wizara ya Afya ni wizara muhimu sana katika taifa lolote. Huwezi kufanya biashara, kulima wala kusoma kama huna afya njema. Afya ndiyo msingi wa uchumi na maendeleo ya taifa,” amesema Dkt. Lyembe. Amesema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora inajiandaa kuanza kutoa huduma za kusafisha figo (dialysis) kwa mara ya kwanza mkoani humo, hatua aliyoeleza kuwa itasaidia kupunguza adha kwa wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo. “Tunategemea ifikapo tarehe 15 ya mwezi ujao kuanza rasmi huduma za dialysis katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa T...

Afya ya Akili Yahitaji Kipaumbele Kama Tulivyopambana na Malaria- Dkt. Lyembe

MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete), Dkt. Joackim Lyembe, ameipongeza Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/2027 akisema imeonyesha dira mpya katika kukabiliana na changamoto za afya ya akili nchini. Akizungumza katika Viwanja vya Bunge Mara baada ya  kufuatia hotuba ya Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, iliyowasilishwa Bungeni jijini Dodoma Mei 11, 2026, Dkt. Lyembe amesema hatua ya Serikali kuhamasisha wananchi kupima afya ya akili ni muhimu kutokana na kuongezeka kwa changamoto za msongo wa mawazo na sonona. “Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kuona suala hili ni moja ya changamoto kubwa zinazohitaji utafiti na nguvu ya pamoja. Zamani tulikuwa tunapoteza watu wengi kwa malaria, lakini sasa ni nadra kusikia mtu amefariki kwa malaria kutokana na maboresho ya huduma za afya na uchunguzi,” amesema Dkt. Lyembe. Ameeleza kuwa maendeleo ya sekta ya afya yameongeza uwezo wa kugundua magonjwa mbalimbali mapema, hali ambayo sa...

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu akutana na Rais wa IFAD, Nairobi

*Wajadili Kilimo himilivu na uendelezaji wa Kilimo Biashara* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 11, 2026 amekutana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Alvaro Lario, jijini Nairobi, Kenya, ambapo wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika sekta ya kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwigulu amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na IFAD katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo himilivu cha tabianchi, maendeleo ya kilimo biashara, mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya kilimo pamoja na uwezeshaji wa vijana na wanawake kiuchumi. Aidha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajia kuendelea kushirikiana na IFAD katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya kilimo ikiwemo mpango wa kuongeza uzalishaji wa alizeti ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa mafuta ya kula nchini. “Kimekuwa ni kikao kizuri kwa sababu tumekuwa na ushirikiano nao kwa muda mrefu, ambapo katika kipindi kilichopita tumeshirikiana nao kat...

Wizara ya Afya Yaomba Kuidhinishiwa Bajeti ya Tril 1.8 Kwa Mwaka wa fedha 2026/27

WAZIRI wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa , ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi trilioni 1.8 kwa ajili ya Matumizi ya Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2026/27 Fungu 52. Waziri wa Afya Mheshimiwa Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 11, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27.  Amesema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni 1.148 ambazo ni sawa na asilimia 64 ya bajeti iliyotengwa zinaombwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, amesema kuwa kati fedha hizo, fedha za ndani ya nchi ni shililingi Bilioni 789.45 na kiasi cha shilingi Bilioni 358.56 zinatoka kwa washirika wa maendeleo.  Mhe.Mchengerwa ameliambia Bunge kuwa, Wizara ya Afya imepanga kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 652.236 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambayo ni sawa na asilimia 36 ya bajeti iliyotengwa.  Amefafanua kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 516, 32...

Serikali yaja na Mageuzi Makubwa Sekta ya afya

WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imejipanga kuendelea kuiboresha Sekta ya Afya nchini kupitia utekelezaji wa vipaumbele mbalimbali vitakavyolenga kuongeza upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi mijini na vijijini. Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo Mei 11, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapitio ya Bajeti ya mwaka 2025/26 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/27. Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuboresha huduma za afya kwa kuimarisha utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, kuongeza wataalam wa afya, pamoja na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya nchini. “Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zenye staha na utu kwa kuboresha mazingira ya utoaji huduma, kupunguza muda wa kusubiri matibabu na kuimarisha mifumo ya kushughulikia malalamiko ya wananchi katika vituo vya afya,” amesema Mhe. Mchengerwa. Katika hatua nyingine, Serikali imeah...