Wizara ya Afya Yaomba Kuidhinishiwa Bajeti ya Tril 1.8 Kwa Mwaka wa fedha 2026/27

GEORGE MARATO TV
0


WAZIRI wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa , ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi trilioni 1.8 kwa ajili ya Matumizi ya Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2026/27 Fungu 52.

Waziri wa Afya Mheshimiwa Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 11, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27. 

Amesema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni 1.148 ambazo ni sawa na asilimia 64 ya bajeti iliyotengwa zinaombwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, amesema kuwa kati fedha hizo, fedha za ndani ya nchi ni shililingi Bilioni 789.45 na kiasi cha shilingi Bilioni 358.56 zinatoka kwa washirika wa maendeleo. 

Mhe.Mchengerwa ameliambia Bunge kuwa, Wizara ya Afya imepanga kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 652.236 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambayo ni sawa na asilimia 36 ya bajeti iliyotengwa. 

Amefafanua kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 516, 323 ni kwa ajili ya mishahara ya Watumishi wa Afya na kiasi cha shilingi Bilioni 135, 913 zitatumika kwa ajili ya matumizi mengineyo.

“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali Watanzania na kuiwezesha Wizara ya Afya kupatiwa fedha nyingi katika miaka mitano iliyopita ambapo Nchi yetu imeendelea kuwa miongoni mwa nchi chache afrika zinazotoa matibabu kwa gharama nafu”amesema Mchengerwa.

Waziri Mchenherwa ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha jumla ya shilingi Trilioni 1.8 katika mwaka wa fedha 2026/27 ambapo amesema kupatikana kwa bajeti hiyo kutasaidia kutekeleza shughuli mbalimbali zilizopangwa ikiwemo vipaumbele vyote 11 ambavyo vimelenga kuiweka Tanzania kuwa mfano kwa utoaji bora wa huduma za afya kwa Wananchi Barani Afrika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top