Afya ya Akili Yahitaji Kipaumbele Kama Tulivyopambana na Malaria- Dkt. Lyembe

GEORGE MARATO TV
0


MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete), Dkt. Joackim Lyembe, ameipongeza Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/2027 akisema imeonyesha dira mpya katika kukabiliana na changamoto za afya ya akili nchini.

Akizungumza katika Viwanja vya Bunge Mara baada ya  kufuatia hotuba ya Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, iliyowasilishwa Bungeni jijini Dodoma Mei 11, 2026, Dkt. Lyembe amesema hatua ya Serikali kuhamasisha wananchi kupima afya ya akili ni muhimu kutokana na kuongezeka kwa changamoto za msongo wa mawazo na sonona.

“Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kuona suala hili ni moja ya changamoto kubwa zinazohitaji utafiti na nguvu ya pamoja. Zamani tulikuwa tunapoteza watu wengi kwa malaria, lakini sasa ni nadra kusikia mtu amefariki kwa malaria kutokana na maboresho ya huduma za afya na uchunguzi,” amesema Dkt. Lyembe.

Ameeleza kuwa maendeleo ya sekta ya afya yameongeza uwezo wa kugundua magonjwa mbalimbali mapema, hali ambayo sasa imeiwezesha jamii kutambua kwa karibu zaidi changamoto za afya ya akili zilizokuwa zikipuuzwa hapo awali.

“Maisha ya sasa yana kasi kubwa sana. Watu wengi wanaonekana wako sawa, lakini afya zao za akili siyo nzuri. Kasi ya maisha, majukumu na mazingira ya sasa vinaongeza changamoto hizi,” amesema.

Dkt. Lyembe amesema kuingizwa kwa huduma za afya ya akili katika vipaumbele vya Serikali kutasaidia kupunguza unyanyapaa uliokuwepo kwa muda mrefu dhidi ya wagonjwa wa afya ya akili.

Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya wizara ya Afya Kwa Mwaka 2026/2027, waziri wa Afya Mohamed Mchenherwa , ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupima afya ya akili, hususan msongo wa mawazo na sonona, akisisitiza kuwa changamoto hizo zinatibika endapo zitagundulika mapema.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, kati ya Julai 2025 hadi Machi 2026 jumla ya watu 254,932 walipatiwa huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia katika vituo vya afya vya msingi nchini, huku upatikanaji wa dawa za afya ya akili ukifikia wastani wa asilimia 75.

Aidha, amesema Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kusaidia kutambua na kuhudumia watu wenye changamoto za afya ya akili, ambapo watu 1,709 walipimwa sonona na 1,362 kubainika kuwa na tatizo hilo na kuendelea na matibabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top