Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Magufuli Alinipigia Simu Saa 8 Usiku Kwamba Haoni Ninachofanya Katika Wizara - Mpina

"Nakumbuka alivyokuwa mfuatiliaji makini wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara, nilipokuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na nilipokuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi simu za usiku na mchana na vikao vingi sana ilikuwa hakuna kulala ni Kazi tu. Nakumbuka siku ameniteua na kuniapisha kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi siku hiyo hiyo usiku saa 8 akanipigia simu akilalamika kwamba haoni ninachofanya katika wizara hiyo. Nilistaajabu sana maana nilikuwa bado hata sijaripoti wizarani na kweli niliamini falsafa yake ya Hapa Kazi tu na kwamba Rais alihitaji kuona mageuzi ya haraka" - Luhaga Mpina "Nilijipanga kufanya kazi za wizara mimi na wenzangu wakati mwingine tulikaa ofisini hadi saa 7 za usiku na baadaye akaanza kutusifia hadharani ikiwemo kutetea msimamo wa kupima samaki kwa rula na kwamba aliamua kutafuta Waziri ambaye atakuwa na kichaa kichaa kama yeye akampata Luhaga Mpina" - Luhaga Mpina Aidha, Mpina amesema wakati Magufuli anafanya zia...

Makamu wa Rais Akiwa Ndani ya Treni ya SGR Kuelekea Morogoro

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisafiri kwa Treni ya Kisasa ya Umeme ya SGR kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro leo tarehe 21 Machi 2026. Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, yatakayofanyika mkoani Morogoro, kesho tarehe 22 Machi 2026.

Waziri wa Ulinzi na Jkt Ashiriki Kikao cha 42 cha Mawaziri wa Sekta ya Ulinzi wa Afrika Mashariki

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 20 Machi, 2026 amewhiriki katika kilele Cha mkutano wa 42 wa Mawaziri wa sekta ya Ulinzi wa jumuiya ya Afrika mashariki kilichofanyika jijini Arusha. Mkutano huu muhimu wa kisekta wa ulinzi umefanyika katika makao makuu ya Afrika mashariki jijini Arusha ukiwa ni muendelezo wa jitihada za kikanda wa kuimarisha ulinzi na usalama miongoni mwa Nchi mwanachama. Ushiriki wa Dkt.Rhimo Nyansaho unadhihirisha dhamira ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tanzania inatoa mchango mkubwa katika kuchangia amani ya kudumu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki, jumuiya za kikanda na kimataifa kwa ujumla , huku ikiweka msisitizo na kipaumbele katika ushirikiano wa kijeshi katika kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazovuka mipaka.  Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Su...

A Helping Hand: Chinese Embassy in Tanzania Supports Rukwa's Healthcare with Free Clinic

By Prosper Makene  In a significant boost to the healthcare sector in Rukwa Region, a free medical clinic has been launched in Sumbawanga Municipality, bringing hope to hundreds of residents who have benefited from the services. The clinic, a result of a partnership between the Tanzanian government and the Chinese Embassy, aims to bring healthcare services closer to the people, addressing the challenges of distance and cost that have long hindered access to medical care. Located at Mazwi Health Centre, the clinic has already made a significant impact, with over 600 people receiving various services, including tests and treatment for diabetes, hypertension, bone diseases, respiratory issues, stomach ulcers, and dental problems, since its opening on March 17, 2026. The services are being provided free of charge, a move that has been welcomed by the local community. Speaking at the launch, Regional Commissioner Charles Makongoro Nyerere hailed the clinic as a significant step towards ...

Ushirikiano wa China-Tanzania: Mamia wapata Huduma za Matibabu Bure Mkoani Rukwa

Na Mwandishi Wetu.  Katika hatua kubwa ya kuboresha sekta ya afya Mkoani Rukwa, kliniki ya matibabu bure imeanzishwa katika Manispaa ya Sumbawanga, ikileta matumaini kwa mamia ya wakazi waliofaidika na huduma hizo.  Kliniki hiyo ambayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Ubalozi wa China, imelenga kuleta huduma za afya karibu na wananchi, ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia Wananchi changamoto za gharama ambazo zimekuwa zikizorotesha huduma za matibabu. Ikiwa katika Kituo cha Afya cha Mazwi, kliniki hiyo imekwisha piga hatua kubwa, ambapo watu zaidi ya 600 wamepata huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vipimo na matibabu ya ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya mifupa, matatizo ya upumuaji, vidonda vya tumbo, na matatizo ya meno, mbapo tangu ifunguliwe Machi 17, 2026. Huduma hizo zinatolewa bure, hatua ambayo imepokelewa vyema na Wananchi.  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere, alisifu klini...

Waziri Kitila Aendelea Kuitangaza Tanzania Nchini China

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo akihutubia Kongamano la Uwekezaji la Weihai katika Jimbo la Shandong.  Prof. Mkumbo amesisitiza kuwa katika kutekeleza Dira 2050, Tanzania inalenga kuwa na uchumi unaotegemea maarifa na ushindani wa kimataifa. Ili kufikia lengo hilo amewahimiza wawekezaji wa China kutotumia mtaji pekee, bali kuleta ujuzi wa mifumo ya kisasa ya teknologia.