Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 20 Machi, 2026 amewhiriki katika kilele Cha mkutano wa 42 wa Mawaziri wa sekta ya Ulinzi wa jumuiya ya Afrika mashariki kilichofanyika jijini Arusha.
Mkutano huu muhimu wa kisekta wa ulinzi umefanyika katika makao makuu ya Afrika mashariki jijini Arusha ukiwa ni muendelezo wa jitihada za kikanda wa kuimarisha ulinzi na usalama miongoni mwa Nchi mwanachama.
Ushiriki wa Dkt.Rhimo Nyansaho unadhihirisha dhamira ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tanzania inatoa mchango mkubwa katika kuchangia amani ya kudumu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki, jumuiya za kikanda na kimataifa kwa ujumla , huku ikiweka msisitizo na kipaumbele katika ushirikiano wa kijeshi katika kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazovuka mipaka.
Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikihakikisha kuwa Amani na Utulivu katika ukanda wa Afrika mashariki ni kichocheo kikubwa cha ustawi wa jamii na maendeleo kwa wananchi takribani milioni 300 kwa Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Kikao hiki kinategemewa kuchochea Kasi ya utekelezaji wa miradi ya usalama na kuimarisha imani ya wananchi na wawekezaji katika ukanda huu kutokana na uhakika wa amani chini ya usimamizi na maelekezo ya wakuu wa Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Kikao cha 42 Cha Mawaziri wa sekta ya Ulinzi wa Afrika mashariki kilitanguliwa na mikutano mbalimbali kuanzia ngazi ya wataalamu wa ulinzi, wakuu wa Majeshi, na makatibu wakuu wa wizara husika kutoka Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Mawaziri wa Ulinzi pamoja na mwenyeji wao , Waziri wa Ulinzi na JKT Tanzania Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho,Wamejadili umuhimu wa Nchi mwanachama kushirikiana katika nyanja za Mafunzo, kubadilishana taarifa za kintelijensia , na kuendesha mazoezi ya kijeshi ya pamoja ili kukabiliana na matishio ya kigaidi pamoja na ushirikiano katika masuala ya afya





