Magufuli Alinipigia Simu Saa 8 Usiku Kwamba Haoni Ninachofanya Katika Wizara - Mpina

GEORGE MARATO TV
0


"Nakumbuka alivyokuwa mfuatiliaji makini wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara, nilipokuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na nilipokuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi simu za usiku na mchana na vikao vingi sana ilikuwa hakuna kulala ni Kazi tu. Nakumbuka siku ameniteua na kuniapisha kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi siku hiyo hiyo usiku saa 8 akanipigia simu akilalamika kwamba haoni ninachofanya katika wizara hiyo. Nilistaajabu sana maana nilikuwa bado hata sijaripoti wizarani na kweli niliamini falsafa yake ya Hapa Kazi tu na kwamba Rais alihitaji kuona mageuzi ya haraka" - Luhaga Mpina

"Nilijipanga kufanya kazi za wizara mimi na wenzangu wakati mwingine tulikaa ofisini hadi saa 7 za usiku na baadaye akaanza kutusifia hadharani ikiwemo kutetea msimamo wa kupima samaki kwa rula na kwamba aliamua kutafuta Waziri ambaye atakuwa na kichaa kichaa kama yeye akampata Luhaga Mpina" - Luhaga Mpina

Aidha, Mpina amesema wakati Magufuli anafanya ziara katika nchi mbali mbali za Afrika alikuwa anaambatana nae kushuhudia talanta aliyopewa na Mungu

"Niliambatana naye kwenye ziara zake za ndani na nje ya nchi, Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia na kushuhudia talanta kubwa aliyopewa na Mwenyezi Mungu" - Luhaga Mpina, Kada wa chama cha ACT Wazalendo katika kumbukizi ya miaka mitano ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli yaliyoadhimishwa Chato Machi 17, 2026

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top