*Karibu Nyumbani Mashujaa Wetu* Habari na Kepten Emanuel Ngonela Hatimaye Kikosi cha Saba cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania kilichokuwa kikihudumu katika mpango wa Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa MINUSCA hatimaye wamefanikiwa kurejea nchini salama Kikosi hicho kimepokelewa leo jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Mapinga na ujumbe kutoka Makao Makuu ya Jeshi ukiongozwa na Brigedia Jeneral George Mwita Itang'are kwa niaba ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jeneral Salumu Haji Othman Akitoa Salamu kwa niaba ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Brigedia Jeneral George Itang'are amesema "Karibuni nyumbani na asanteni kwa kutuwakilisha vyema kama Jeshi na nchi kwa ujumla pamoja na changamoto ndogo ndogo za kiutawala mlizokuwa nazo mliweza kutekeleza jukumu hili vyema" Brigedia Jenerali Itang'are amesema kuwa Jeshi linatambua kuwa kupitia ushiriki wa...
Marato tv - Sauti ya Jamii