*Karibu Nyumbani Mashujaa Wetu*
Habari na Kepten Emanuel Ngonela
Hatimaye Kikosi cha Saba cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania kilichokuwa kikihudumu katika mpango wa Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa MINUSCA hatimaye wamefanikiwa kurejea nchini salama
Kikosi hicho kimepokelewa leo jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Mapinga na ujumbe kutoka Makao Makuu ya Jeshi ukiongozwa na Brigedia Jeneral George Mwita Itang'are kwa niaba ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jeneral Salumu Haji Othman
Akitoa Salamu kwa niaba ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Brigedia Jeneral George Itang'are amesema "Karibuni nyumbani na asanteni kwa kutuwakilisha vyema kama Jeshi na nchi kwa ujumla pamoja na changamoto ndogo ndogo za kiutawala mlizokuwa nazo mliweza kutekeleza jukumu hili vyema"
Brigedia Jenerali Itang'are amesema kuwa Jeshi linatambua kuwa kupitia ushiriki wa kikosi hicho katika mpango wa ulinzi wa amani umewezesha kupatikana kwa uzoefu kutokana na mambo matatu ambayo ni nguzo za Mwanajeshi ambazo ni utiifu uaminifu na uhodari na kuishi katika viapo vyetu Kama Mwanajeshi.
Aidha amewakumbusha kutumia mitandao ya kijamii kwa namna chanya ikiwemo kujielimisha,kuendelea kutekeleza majukumu yenu Vikosini mwenu kwa ari mpya sanjari na kuwataka mkaungane na familia zenu hasa kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwishoni mwa mwaka.
Kwa Upande wake,Kamanda Kikosi hicho kilichomaliza jukumu lake Luteni Kanali Joseph Mushilu amekabidhi cheti ambacho Kikosi kilitunukiwa na Umoja wa Mataifa kufuatia kutambua mchango wa Kikosi hicho katika kuwalinda Raia wa Jamhuri ya Africa ya Kati na kuimarisha hali ya usalama nchini humo.
Kikosi hicho kilichokuwa na Maafisa na Askari zaidi ya Mia tano sitini Kati yao walikuwa ni Askari wa Kike.
Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa na umekuwa ikichangia Walinda Amani , Maafisa Wanadhimu na Watalaam wa Wakijeshi sehemu mbalimbali Dunia ambako kwa sasa,Walinda amani kutoka Tanzania wako katika nchi za Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu Kongo, Msumbiji, Lebanon na Jamhuri ya Afrika ya Kati.