Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga leo Disemba 22, 2024 amegawa hati za nyumba, funguo za nyumba, majiko ya gesi pamoja na miti ya matunda Kwa kaya 89 za walioathirika wa maporomoko ya tope ya mlima Hanang kwa ambao hawakupatiwa hati wakati wa ufunguzi wa nyumba hizo.
RC Sendiga, amefanya zoezi hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa Disemba 20, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Makazi hayo Mapya ya waathirika wa maporomoko ya matope.
Akizungumza na wanufaika wa nyumba hizo RC Sendiga amewaasa kuishi kwa upendo na amani, wanapaswa kuzitunza nyumba hizo ikiwemo kuzingatia usafi na kuboresha mazingira yanayowazunguka.
Baadhi ya wanufaika wa nyumba hizo wametoa shukrani zao kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kuwa wamezifurahia huku wakiahidi kuzitunza na kutunza mazingira hayo.