Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DUCE NA GEL KUWATAFUTIA FURSA VIJANANA

Na Mwandishi Wetu Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) na Wakala wa Elimu Nje ya Nchi Global Education Link (GEL) wamesaini ya kuwatafutia fursa  mbalimbali za kilaaluma wanafunzi a chuo hicho. Makubaliano hayo yalisainiwa jana jijini Dar es Salaam baina ya  Mkurugenzi Mkuu wa GEL, Abdulmalik Mollel na kaimu Mkuu wa chuo hicho, Profesa  Pendo Malangwa. Akizungumza kwenye hafla hiyo, mgeni rasmi ambaye alimwakilisha Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Geofrey Kituye  aliipongeza GEL na DUCE kwa kuona umuhimu wa kuingia makubaliano hayo.                                   “Nitumie fursa hii kuwapongeza sana DUCE pamoja na Global Education Link kwa kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kusaidia maendeleo ya elimu na maandalizi ya vijana wetu kwa maisha ya kazi baada ya hatua mbalimbali za masomo,” alisema Kituye. Aidha, alisema Dar es Salaam ni mkoa wenye nafasi kubwa s...

Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jkt Kusomwa Kesho Mei 19-2026

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. *Dkt. Rhimo Nyansaho, (Mb)* amewasilisha hati za randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026 /2027.  Uwasilishaji rasmi wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 utafanyika kesho Jumanne Mei 19, 2026 bungeni jijini Dodoma.

Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jkt Kusomwa Kesho Mei 19-2026

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. *Dkt. Rhimo Nyansaho, (Mb)* amewasilisha hati za randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026 /2027.  Uwasilishaji rasmi wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 utafanyika kesho Jumanne Mei 19, 2026 bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Amuaga Mkurugenzi Mkazi wa Benki Ya Dunia Kanda ya Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe

▪️Apongeza mchango wake katika maendeleo nchini. WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 17, 2026 ameshiriki katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Kanda ya Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Nathan Belete, iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Mwigulu alimpongeza Nathan kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia pamoja na kuunga mkono juhudi za maendeleo katika sekta mbalimbali nchini. Amesema kuwa imeshuhudiwa ongezeko kubwa na la kihistoria la ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia, ambapo takribani dola za Marekani bilioni 4.27 zilipatikana kupitia miradi na programu mbalimbali. “Niruhusuni kwa mara nyingine kutoa shukrani zangu za dhati kwa Nathan kwa huduma yake ya kujitolea na mchango wake mkubwa katika safari ya maendeleo ya Tanzania, na kumtakia mafanikio mema katika majukumu yake mapya,” amesema Dkt. Mwigulu. Aliongeza kuwa m...

Kazala: Migogoro ya Ardhi Kero Kubwa Kasulu Vijijini

MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Mhe. Edibilly Kazala amesema ameendelea kuwa karibu na wananchi kupitia mikutano ya hadhara inayolenga kusikiliza changamoto zao na kutafuta suluhisho la kudumu kwa kushirikiana na Serikali. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 17, 2026, Mhe. Kazala amesema tangu achaguliwe ameweza kufanya zaidi ya mikutano 50 ya kuzunguka na kufungua maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, huku baada ya uchaguzi akifanya tena mikutano 58 ya kuwashukuru wananchi kwa imani waliyoionesha pamoja na kupokea kero zao moja kwa moja. Amesema kero kubwa inayowakabili wananchi wengi wa Kasulu Vijijini ni migogoro ya ardhi, hususan katika maeneo ya vijijini, ambapo wananchi wamekuwa wakikumbana na changamoto za mipaka, matumizi ya ardhi pamoja na maeneo ya makazi na shughuli za kilimo na ufugaji. “Migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikiwatesa wananchi kwa muda mrefu, lakini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha wananchi wanapatiwa haki zao...

Dkt. Mwigulu Awahakikishia Wananchi Kasi ya Utekelezaji wa Miradi

_▪️ Asema utekelezaji wa Bwawa la Farkwa kuanza baada ya kukamilika kwa taratibu za manunuzi_ _▪️ Aagiza kukomeshwa kwa ukamataji usio na msingi wa vitendea kazi vya wananchi_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miradi yote ya maendeleo iliyopungua kasi ya utekelezaji inaanza tena kutekelezwa kwa kasi inayotakiwa ili wananchi waendelee kunufaika na huduma za kijamii na kiuchumi. Amesema hayo leo Jumapili, Mei 17, 2026, alipowahutubia wananchi wa Wilaya ya Chemba katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kambi ya Nyasa, akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi. Dkt. Mwigulu amesema baadhi ya miradi ilipungua kasi baada ya Serikali kuelekeza nguvu kubwa katika kukamilisha miradi ya kimkakati ya kitaifa iliyokuwa imefikia hatua za mwisho, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, reli ya kisasa pamoja na Daraja la Kigongo–Busisi.  “Kilichosababisha baadhi ya miradi kupungua kasi haikuwa uzembe wala kupuuza. Ilikuwa ni mka...