MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Mhe. Edibilly Kazala amesema ameendelea kuwa karibu na wananchi kupitia mikutano ya hadhara inayolenga kusikiliza changamoto zao na kutafuta suluhisho la kudumu kwa kushirikiana na Serikali.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 17, 2026, Mhe. Kazala amesema tangu achaguliwe ameweza kufanya zaidi ya mikutano 50 ya kuzunguka na kufungua maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, huku baada ya uchaguzi akifanya tena mikutano 58 ya kuwashukuru wananchi kwa imani waliyoionesha pamoja na kupokea kero zao moja kwa moja.
Amesema kero kubwa inayowakabili wananchi wengi wa Kasulu Vijijini ni migogoro ya ardhi, hususan katika maeneo ya vijijini, ambapo wananchi wamekuwa wakikumbana na changamoto za mipaka, matumizi ya ardhi pamoja na maeneo ya makazi na shughuli za kilimo na ufugaji.
“Migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikiwatesa wananchi kwa muda mrefu, lakini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha wananchi wanapatiwa haki zao na migogoro hiyo inapatiwa ufumbuzi wa kudumu,” amesema Mhe. Kazala.
Mje. Kazala ameambatana na Naibu waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi katika Jimbo la kasulu vijijini Kwa lengo la kueasikilixa wananchi na kutatua kero walizonazo kama sehemu ya ahadi aliyowaahidi wananchi ho wakati wa uchaguzi.
Kadhalika,Mhe. Kazala amesema yupo tayari kuwatumikia wananchi wake ambapo amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitumia utu kwa kuwajali na kiwathamini wananchi wa Tanzania.





Comments
Post a Comment