Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DUCE NA GEL KUWATAFUTIA FURSA VIJANANA


Na Mwandishi Wetu

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) na Wakala wa Elimu Nje ya Nchi Global Education Link (GEL) wamesaini ya kuwatafutia fursa  mbalimbali za kilaaluma wanafunzi a chuo hicho.

Makubaliano hayo yalisainiwa jana jijini Dar es Salaam baina ya  Mkurugenzi Mkuu wa GEL, Abdulmalik Mollel na kaimu Mkuu wa chuo hicho, Profesa  Pendo Malangwa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, mgeni rasmi ambaye alimwakilisha Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Geofrey Kituye  aliipongeza GEL na DUCE kwa kuona umuhimu wa kuingia makubaliano hayo.

                     
           

“Nitumie fursa hii kuwapongeza sana DUCE pamoja na Global Education Link kwa kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kusaidia maendeleo ya elimu na maandalizi ya vijana wetu kwa maisha ya kazi baada ya hatua mbalimbali za masomo,” alisema Kituye.

Aidha, alisema Dar es Salaam ni mkoa wenye nafasi kubwa sana katika maendeleo ya taifa kwani una idadi kubwa ya ya watu, shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi, vyuo vya elimu ya juu, hospitali za rufaa na za binafsi, pamoja na viwanda vikubwa na vya kati vinavyoendelea kukua kila siku.

Alisema ukuaji huo wa uchumi na miundombinu una maana moja kubwa sana kwa wadau wa elimu kwani unamaanisha  kuna wajibu wa kuandaa vijana wenye maarifa, ujuzi, maadili, na uwezo wa kutumia fursa zinazozidi kuongezeka katika mkoa huo na taifa.

“Ndiyo maana suala la kunasihi vijana kuhusu ulimwengu wa kazi baada ya masomo lina umuhimu mkubwa sana katika kipindi hiki. Kimsingi, mwanafunzi wa leo anatakiwa kujitambua mapema hususani kuelewa uwezo wake, mahitaji yake, ndoto zake, na fursa za kazi zilizopo mbele yake,” alisema

Alisema kijana anatakiwa kusoma akiwa anajua anasoma nini, kwa nini, na anakwenda kutumia vipi maarifa na ujuzi alioupata.

Alisema bila  mwongozo sahihi wa taaluma, vijana wengi wanaweza kuchagua masomo bila kulinganisha matamanio yao, uwezo wao na mahitaji ya soko la ajira au fursa zinazokuja katika miaka ijayo.

“Kwa kuzingatia hilo, ni jambo la faraja kuona kuwa DUCE pamoja na Global Education Link wameamua kuunganisha nguvu katika eneo hili muhimu,” alisema.

“Kwa niaba ya Ofisi ya Elimu Mkoa wa Dar es Salaam napenda kuupongeza tena uongozi wa DUCE pamoja na Global Education Link kwa kuanzisha ushirikiano huu muhimu. Ni imani yangu kuwa hatua hii ni mwanzo wa mabadiliko makubwa katika namna tunavyowaandaa vijana wetu kwa elimu, ajira, ubunifu, na maisha ya baadaye,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel alisema  GEL imefikisha miaka 19 katika kufanyakazi ya kuwapa wanafunzi mwongozo wa taaluma za kusomea.

                  

Alisema kazi kubwa ambazo wanafanya ni kuwatafutia wanafunzi wa Tanzania kupata fursa za kusoma nje ya nchi na kusaidia ushirikiano baina ya vyuo vikuu vya ndani nan je ili kuchukua teknolojia kwenye nchi hizo.

Alisema nchi zilizoendelea zimefika hapo kutokana na maarifa makubwa ya wananchi wake hivyo GEL imeona umuhimu wa kuchukua maarifa hayo yaje kusaidia hapa nchini Tanzania.

                                

Alisema GEL imesaini mikataba kama hiyo na vyuo vikuu vya Dodoma, Mzumbe, Nelson Mandela, TIA na vingine na kwamba kusaini na DUCE ni mwendelezo wa utaratibu huo.                                                         

“Kila chuo tunachosaini makubaliano tunakuwa na malengo maalum nacho, leo tumesaini na DUCE kwaajili ya mwongozo kwa wanafunzi na hatuishii kwa wanafunzi, wazazi ambao wanataka kujiendeleza kielemu au walimu wanaotaka kujiendeleza tunawapa mwongozo,” alisema Mollel. 

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Profesa  Pendo Malangwa alisema tukio hilo linaonyesha dhamira ya dhati ya kuwaaandaa vijana kwenye maisha ya taaluma na hatimaye ajira siku za baadae.

                              

Alisema kupitia ushirikiano huo wanafunzi wa chuo hicho watapata mwongozo wa kitaaluma na kuelewa fursa zilizoko ndani nan je ya nchi kwaajili ya kupambana na ushindani unaokua kwa kasi ulimwenguni kwenye soko la ajira.

Alisema DUCE inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kutoa elimu bora, kufanya tafiti na kuandaa wataalamu na kwamba GEL itaweka uzoefu wake kwa kuwaunganisha vijana kwa kuwapa ushauri na maendeleo ya kitaaluma. 

                               

Tunatarajia kuongeza mwongozo wa kitaaluma na ushirikishwaji wa wanafunzi na kuwajengea uwezo na kuimarisha mawasiliano kupitia vyombo vya habari ili kusaidia vijana kuelewa taaluma mbalimbali na mahitaji ya soko la ajira. 

                                    

“Sote ni mashahidi hapa vijana wengi wakimaliza kidato cha sita hawana uwezo wa kuchagua wanachotaka kusoma, wengine wanachagua tu kwasababu walisikia, sasa kupitia ushirikiano huu tunataka vijana wachague kitu wanachokijua kitakacholeta tija kwenye maisha yao ya baadae,” alisema. 













Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...