Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesisitiza kuwa mafanikio yake katika tafiti, ufundishaji na utoaji wa huduma kwa jamii yanategemea kwa kiasi kikubwa mchango wa wafanyakazi wake, huku kikiahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ili kuongeza tija na ustawi kazini. Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Raphael Chibunda, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Amandus Muhairwa, amesema uongozi wa Chuo umejipanga kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi na kuimarisha mazingira rafiki ya utendaji kazi. Akijibu risala ya wafanyakazi, Prof. Muhairwa alieleza kuwa Menejimenti imepokea kwa uzito maoni, changamoto na mapendekezo yaliyowasilishwa, na itaendelea kuyafanyia kazi kupitia mifumo rasmi ya uongozi kwa lengo la kupata suluhisho endelevu. Alibainisha kuwa SUA inaendelea kuboresha upatikanaji wa vitendea kazi kwa kuimarisha mifumo ya manunuzi na kush...