Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mavunde ni mfano wa kuigwa - Femata

  WIZARA ya Madini,imesema itaendelea na juhudi za kuwarasimisha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayowahamasisha kufanya uwekezaji. Hayo yameelezwa leo Mei 2,2025 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Madini,Anthony Mavunde bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026. Waziri Mavunde amesema Serikali itaendelea kuhamasisha taasisi za kifedha kutoa mikopo ya fedha na vifaa kwa wachimbaji wadogo. Vilevile, kuboresha utendaji wa vituo vya mfano ili kuimarisha utoaji wa huduma na mafunzo kwa wachimbaji wadogo na kuimarisha huduma za uchorongaji kwa wachimbaji wadogo.  “Wizara pia itaimarisha utekelezaji wa mipango ya kuwawezesha wachimbaji wadogo ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija kwa kuwatengea maeneo na kuwapatia leseni kwenye maeneo ambayo yana taarifa za jiolojia. “Kuhamasisha wachimbaji wadogo kushiriki mikutano, maonesho na makongamano mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujifu...

Hotuba Bajeti ya Wizara ya Madini 2025/26

  *Watendaji, watumishi, wageni, wananchi na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini wamewasili katika Viwanja vya Bunge,  Jijini Dodoma kwa ajili ya kufuatilia Uwasilishaji wa Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2025/2026 unaowasilishwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde,  leo Mei 2, 2025*

Serikali ya Tanzania yakanusha ukiukwaji wa Sheria kesi ya Lissu kusikilizwa kwa mtandao

  Serikali ya Tanzania imesema hakuna sheria iliyokiukwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ilipoamua kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kwa njia ya mtandao. Hayo yameelezwa Ijumaa Bungeni mjini Dodoma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2025/26. “Ukifuatilia kilichotokea tarehe 24, Procedures (taratibu) zile zilikuwa properly lollowed (zimefuatwa inavyotakiwa), sasa huyu mtu anayetokea anayesema kuna uvunjifu wa sheria, sheria ipi sheria si ndiyo hii?,” alihoji Johari na kuongeza: “hii ndiyo sheria, na mimi ninayezungumza hapa ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” Akifafanua zaidi, Johari alisema Mahakama inaweza kuendesha kesi kwa njia ya mtandao iwapo imeona kuna tishio lolote baada ya kufanya tathmini. “Mahakama itaassess (tathmini) mazingira yaliyopo siku hiyo na kuona kwamba tuisikilizeje shauri hili na hasa kama kuna mazing...

Bilioni 2 zalipa malimbikizo ya posho malipo ya likizo watumishi mkoani Mara

Na Shomari Binda-Musoma  ZAIDI ya shilingi bilioni 2 zimelipa stahiki malimbali zikiwemo za posho mishahara na malipo ya likizo kwa watumishi wa umma mkoani Mara. Malipo hayo yamefanywa na serikali kuu yakiwa ni katika kipindi cha mwaka 2024/2025 na kuongeza ari ya kufanya kazi. Hayo yamesemwa leo mei mosi na Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi katika sherehe za wafanyakazi zilizofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo. Amesema serikali inatambua mchango wa wafanyakazi na ipo tayari kujibu hoja zao ikiwemo ulipaji wa madeni. Kanali Mtambi amesema wakati serikali ikitekeleza haki wafanyakazi wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa kuwahudumia wananchi. Amesema wakati hayo yakitendeka waajili wahakikishe michango ya watumishi inawasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati. "  Serikali inatambua mchango wa watumishi na ndio inapelekea madai yenu yanalipwa na maisha yanaendelea. " Nitumie nafasi hii pia kuagiza taasisi zote kufanya vikao vya mabaraza ya wafany...

Wafanyakazi Le Grand Hotel washerehekea Mei Mosi na kuahidi huduma bora

Na Shomari Binda-Musoma  WAFANYAKAZI wa Le Grand Victoria Hotel ya mjini Musoma wamesherehekea sherehe za mei mosi na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja. Huduma ambazo wamewahakikishia wateja ni kuhakikisha kuanzia mapokezi na kuwapz huduma bora za malazi,chakula na vinywaji. Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye sherehe hizo zilizofanyika hotelini hapo wamesema mteja anapohudumiwa vizuri hawezi kwenda mahala pengine na wao wapo tayari kutoa huduma bora. Mmoja wa wafanyakazi wa Hotel hiyo Rukia Maulidi amemshukiru mkurugenzi wa hotel hiyo Ramadhan Msomi kwa kuwaandalia sherehe za mei mosi na kukutana kwa pamoja. Amesema suala huduma bora kwao ni kipaumbele na kuwakaribisha wageni wote watakaofika Musoma kwaajili ya kuhudumiwa ndani ya Hotel hiyo. " Tunamshukuru mkurugenzi wetu kwa lutuandalia hsfla hii ya sherehe za mei mosi na kutukutanisha wsfanyakazi wote pamoja " Wateja wetu tunawaahidi huduma bora pale watakapotutembelea wakiwa kwenye mji wa Musoma wakati w...