Wafanyakazi Le Grand Hotel washerehekea Mei Mosi na kuahidi huduma bora

GEORGE MARATO TV
0



Na Shomari Binda-Musoma 

WAFANYAKAZI wa Le Grand Victoria Hotel ya mjini Musoma wamesherehekea sherehe za mei mosi na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.


Huduma ambazo wamewahakikishia wateja ni kuhakikisha kuanzia mapokezi na kuwapz huduma bora za malazi,chakula na vinywaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye sherehe hizo zilizofanyika hotelini hapo wamesema mteja anapohudumiwa vizuri hawezi kwenda mahala pengine na wao wapo tayari kutoa huduma bora.

Mmoja wa wafanyakazi wa Hotel hiyo Rukia Maulidi amemshukiru mkurugenzi wa hotel hiyo Ramadhan Msomi kwa kuwaandalia sherehe za mei mosi na kukutana kwa pamoja.

Amesema suala huduma bora kwao ni kipaumbele na kuwakaribisha wageni wote watakaofika Musoma kwaajili ya kuhudumiwa ndani ya Hotel hiyo.

" Tunamshukuru mkurugenzi wetu kwa lutuandalia hsfla hii ya sherehe za mei mosi na kutukutanisha wsfanyakazi wote pamoja

" Wateja wetu tunawaahidi huduma bora pale watakapotutembelea wakiwa kwenye mji wa Musoma wakati wowote",amesema.

Kwa upande wake meneja wa hotel hiyo Paul Mutinda amesema kwa sasa wameanzisha huduma ya utalii wa maji kupitia boti za kisasa ndani ya ziwa Victoria ili kuwafikia wateja wao.

Amesema ili kuhakikisha huduma bora zinaendelea kutolewa suala la elimu kwa wafanyakazi inatolewa Mara kwa mara ili kuwahifumia wateja vixuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top