Bilioni 2 zalipa malimbikizo ya posho malipo ya likizo watumishi mkoani Mara

GEORGE MARATO TV
0



Na Shomari Binda-Musoma 

ZAIDI ya shilingi bilioni 2 zimelipa stahiki malimbali zikiwemo za posho mishahara na malipo ya likizo kwa watumishi wa umma mkoani Mara.

Malipo hayo yamefanywa na serikali kuu yakiwa ni katika kipindi cha mwaka 2024/2025 na kuongeza ari ya kufanya kazi.

Hayo yamesemwa leo mei mosi na Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi katika sherehe za wafanyakazi zilizofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo.

Amesema serikali inatambua mchango wa wafanyakazi na ipo tayari kujibu hoja zao ikiwemo ulipaji wa madeni.


Kanali Mtambi amesema wakati serikali ikitekeleza haki wafanyakazi wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa kuwahudumia wananchi.

Amesema wakati hayo yakitendeka waajili wahakikishe michango ya watumishi inawasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati.

"  Serikali inatambua mchango wa watumishi na ndio inapelekea madai yenu yanalipwa na maisha yanaendelea.

" Nitumie nafasi hii pia kuagiza taasisi zote kufanya vikao vya mabaraza ya wafanyakazi ili kuzungumza masuala ya kazi",amesema.

Akisoma risala ya wafanyakazi kwenye sherehe hizo mmoja wa waratibu Grace Martine ameishukuru serikali kwa kujibu hoja za wafanyakazi zilizotolewa mwaka 2024.


Amesema wafanyakazi wapo tayari kuendeleza kufanya kazi kwa kuwa inawatekelezea mahitaji yao.


Sherehe za mei mosi kimkoa zimefanyika manispaa ya Musoma na kuhudhuriwa na wafanyakazi kutoka Wilaya zote za mkoa wa Mara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top