▪️Waziri Mavunde asisitiza ushirikiano kwenye utafiti wa madini na uongezaji wa thamani madini ▪️Korea yaonesha utayari kuwekeza nchini katika uendelezaji wa madini mkakati ▪️Serikali ya Tanzania kuandaa mkakati maalum wa uvunaji na uendelezaji wa Madini Mkakati ▪️Wawekezaji wa Viwanda vya kuongeza thamani madini wakaribishwa 📍Dar es Salaam Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Jamhuri ya Korea katika kutekeleza mkakati wake wa kuendeleza madini mkakati na muhimu nchini. Hayo yamesemwa leo tarehe 24 Januari, 2025 na Waziri wa Madini, *Mhe. Anthony Mavunde* alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea nchini Tanzania, *Mhe. Eunju Ahn* katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. "*Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* alitupa maelekezo mahsusi ya kuhakikisha rasilimali hii ya madini mkakati tunaiwekea mfumo thabiti ili Nchi yetu ipate manufaa zaidi. Mkakati wa uvunaji madini ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika umelenga kutimiza...
Marato tv - Sauti ya Jamii