Na Hamida Ramadhan, Rukwa NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Kwela, Mhe. Deus Sangu amewaomba Wananchi wasisahau maendeleo wanayoyaona katika Jimbo hilo ni kutokana na jitihada za Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hayo ameyasema leo kwenye mkutano wa kampeni za Serikali za Mitaa uliofanyika katika Kijiji cha Ilemba, Kata ya Kalambanzite katika Jimbo la Kwela mkoani Rukwa. Aidha, amefafanua kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, kata ya Kalambanzite imeimarika katika Sekta ya Afya, Elimu, Barabara, Maji pamoja na Umeme. Amewataka Wananchi hao kujitokeza ifikapo Novemba 27 mwaka huu ili kuchagua Viongozi wenye maono na mwelekeo wa kuwaunganisha kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa ambao ni Wagombea kupitia CCM. " Chagueni Viongozi ambao wana uelewa wa matatizo na kujua namna ya kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi pasipo kuj...
Marato tv - Sauti ya Jamii