Maafisa Watendaji wa Kata wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wametakiwa kuhamasisha Kilimo Cha Mazao ya Chakula na mbogamboga katika Mashamba ya Shule za Msingi na Sekondari ili kukabiliana na kupunguza tatizo la Lishe Mashuleni.
Mkuu wa wilaya hiyo Johari Samizi amesema kuwa hatua hiyo itawezesha wanafunzi kupata Chakula Cha kutosha shuleni na hivyo kuondoa Tatizo la utoro na hatimaye kuinua kiwango cha ufaulu.
Kikao hicho kimejadili Hali ya Maendeleo ya Lishe kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari
Akiwasilisha Taarifa ya Maendeleo na utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika Halmashauri ya Misungwi Afisa Lishe Bi. Lucy ameeleza kwamba Juhudi zinaendelea kuboreshwa ili kuhakikisha suala la Lishe kwa Wanafunzi linapatiwa kipaumbele
Lucy amebainisha hivi sasa Shule nyingi zinaendelea kutoa Chakula angalau mara moja kwa mlo mmoja kwa siku kupitia Makubaliano ya Michango ya Chakula kupitia Wazazi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Addo Missama amewataka Watendaji wa vijiji na Kata pamoja na Wataalam kuongeza bidii katika kuhakikisha Maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita kuhusu Lishe yanazingatiwa na kutekelezwa kikamilifu ukiwemo Mkataba wa Lishe.






Comments
Post a Comment