Mkazi wa wa Kashishi kata ya Nyamhongolo wilayani Ilemela Mkoani Mwanza Athanas Masubo amekanusha madai ya kumbaka Mama Mmoja mwenye Umri wa miaka 68.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Masubo amesema kuwa Tuhuma zinazoelekezwa kwake hazina ukweli wowote bali zinalengo la kumchafua.
Masubo amehusisha Tuhuma hizo na Shauri la Jinai namba 1980/2024 katika Mahakama ya Mwanzo Mjini Wilaya nyamagana lilomhusisha Mlalamikaji Joseph Mushi na Mshtakiwa Kazimiri Matono ambaye alishtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kinyume na kifungu 89(1) Sura 16 K/A R. E 2019.
Katika Shauri hilo,Masubo alikuwa shahidi namba mbili ambapo kwenye ushahidi wake alieleza kuwa August 13 Mwaka huu akiwa amekaa Majukano hotel na Mlalamikaji na watu wengine alimpigia Mshtakiwa maarufu kama Bonge simu amfuate akiwa na bodaboda na alipofika na kumuona Mlalamikaji alianza kumtukana.
Baada ya ushahidi wa mashahidi watatu,Mshtakiwa Kazimiri Matono alipatikana na hatia ambapo Hakimu Mkazi Nkwabi wa Mahakama ya wilaya nyamagana alimhukumu kifungo cha siku sitini gerezani ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.
Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa oktoba 30 mwaka huu,Baadhi ya madereva wa bodaboda wanadaiwa kuapa kulipiza kisasi dhidi ya watu waliotoa ushahidi dhidi ya bodaboda mwenzao.
Katika kutimiza azma yao,Bodaboda hao wanadaiwa kumtumia Mama wa Kiongozi wa Bodaboda kwenye Mtaa wa Kashishi Sohela Waryoba anayedai kubakwa.
Kando ya Bodaboda hao kudaiwa kuapa kulipiza kisasi,pia masuala ya kisiasa nayo yanatajwa kuwa nyuma ya sakata hilo.
Akizungumzia Tukio hilo Novemba 13 Mwaka huu,Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi dhidi ya Tuhuma zunazomkabili Athanas Masubo na Tayari amehojiwa kuhusu Tuhuma hizo.
Kwa mujibu wa Mutafungwa,Tukio hilo linadaiwa kutendeka nyumbani kwa Masubo
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps

Comments
Post a Comment