Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Biteko ashiriki uapisho wa Rais Duma Boko Botswana

*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Novemba 8, 2024 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za uapisho wa Rais wa sita wa Botswana, Mhe. Gedion Duma Boko. Katika uapisho huo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa wa nchi hiyo, umeshuhudiwa na mamia ya wananchi wa Botswana na vitongoji vyake wakiwemo marais na viongozi wa wakuu kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Rais mteule wa Jamhuri ya Botswana ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Sita wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ambapo ameahidi kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na sheria za nchi hiyo. Aidha amesema atatekeleza majukumu yake ya kazi akijielekeza katika kuleta maendeleo na Usatawi wa Nchi na Wananchi wake. Akihutubia taifa kwa mara ya kwanza Rais Boko amesema anajivunia taifa lake la Botswana huku akiongeza kuwa matokeo ya ushindi na wake ni tukio la kihist...

Waziri Mkuu Aahirisha Bunge na kutoa Maagizo mazito kwa watendaji wa serikali

  -Atoa wito watendaji serikalini watafsiri vema vipaumbele vilivyoanishwa kwenye Mpango wa Maendeleo WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wote Serikalini wahakikishe vipaumbele vilivyoanishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/2026 vinatafsiriwa vema kwenye mipango ya Taasisi zao. Amesema mpango huo umejikita katika kuendeleza na kukamilisha utekelezaji wa afua zinazotoa matokeo ya maeneo matano ya kipaumbele ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 8, 2024) wakati akiahirisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 12 Bungeni jijini Dodoma, ambapo amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) iliwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/2026. “Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi itaweka mkazo katika maeneo ya miradi ya kielelezo yenye manufaa na matokeo makubwa na kujielekeza katika vipaumbele vya mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/2026.” Amesema vi...

Wakulima Bugwema Waeleza Jinsi Kilimo cha Umwagiliaji Kwa Kutumia Pampu za Mafuta Kinavyowapa Hasara

Na Emmanuel Chibasa 🚨Kila siku wanakodi jenereta na Pampu Kwa Shilingi 10,000 🚨Wanatumia kuanzia Lita 3 Hadi 20 Kwa siku Kumwagilia shamba la ekari 1 Hadi 3 🚨Lita Moja ya mafuta Bugwema inauzwa shilingi 4000 🚨Wadai Kuuziwa Pembejeo Zisizo na ubora Katika mipira ya umwagiliaji, Mbegu pamoja na dawa. WAKULIMA wadogo wanaotegemea kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia Pampu zinazoendeshwa na mafuta kando kando ya ziwa Victoria, katika kijiji cha Bugwema kata ya Bugwema Musoma Vijijini Mkoani Mara, Wanadai kutumia gharama kubwa kutokana kukosa teknolojia nafuu, hali inayopelekea kupata hasara na kushindwa kulima kilimo cha umwagiliaji kwa tija. Wakulima hawa wanaeleza kuwa wamekua wakitumia fedha nyingi kununua mafuta ya dizeli na petroli kwa ajili ya kuendesha pampu zinazotumika kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria. Hali hii imesababisha hasara kwa wakulima wengi, huku wakiwa na ndoto ya kuboresha uzalishaji wao na kuleta tija katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji. Wakizungumza na Geor...

Tanzania yang'ara miradi ya kinywe

*Ripoti ya Benki ya Dunia Yaitaja ya Tatu Afrika, Sita Duniani* *Tanzania yatoa Somo mwelekeo sahihi nchi za Afrika katika Uwekezaji, uvunaji wenye maslahi kwa Wananchi* *Yasisitiza ushirikiano baina ya nchi za Afrika* *Capetown* Ripoti ya Benki ya Dunia na Takwimu za Taasisi ya Jiolojia ya Marekani kuhusu makisio ya utajiri wa mashapo ya Madini ya Kinywe ifikapo mwaka 2050 imeitaja nchi ya  Tanzania kushika nafasi ya Sita (6) Duniani na nafasi ya Tatu (3) Afrika huku Msumbiji ikishika nafasi ya kwanza  ikifuatiwa na Madagasca  kwa upande wa nchi za Afrika. Hayo yamebainishwa Novemba 7, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance wakati akimwakilisha Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde katika mjadala wa Mawaziri 'Ministerial session' uliofanyika katika Kilele cha Mkutano wa Madini Muhimu Afrika uliofanyika Cape Town, Afrika Kusini na kuongeza kwamba, Tanzania imebarikiwa kuwa na aina nyingi za madini muhimu yanayohitajika kwa ajili ...

Rais mteule Donald Trump amemteua mwenyekiti-mwenza wa timu yake ya kampeni, Susie Wiles, kuwa White House Chief of Staff wa Marekani

 Rais mteule Donald Trump amemteua mwenyekiti-mwenza wa timu yake ya kampeni, Susie Wiles, kuwa White House Chief of Staff wa Marekani. Anakua mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo. Nafasi ya WH Chief of Staff ni moja ya nafasi zenye ushawishi mkubwa katika utawala wa Marekani, ambapo mhusika huyu hutumika kama mshauri mkuu wa rais na kuhakikisha utendaji wa Ikulu unafanyika kwa ufanisi. Haya ni baadhi ya majukumu ya nafasi hii: 1. Ratiba na Mipangilio: Anasimamia ratiba ya kila siku ya rais, akihakikisha kuwa mikutano na majukumu yote yanazingatia malengo ya utawala. 2. Mshauri na Mlinda Mlango: Akiwa mshauri wa karibu zaidi wa rais, anahusika na kuchuja taarifa na watu wanaofika kwa rais ili kuhakikisha muda na nishati ya rais vinatumika vyema. 3. Mkurugenzi ya Sera na Watumishi: Anasimamia washauri wakuu na watumishi wa Ikulu, akihakikisha kuwa wote wanashirikiana katika kufanikisha ajenda na sera za rais. 4. Kujenga Mahusiano Muhimu: Akitumika kama kiunganishi kati ya ...

Ccm Misungwi yajizatiti kuyavunja makundi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

    Chama chamapinduzi(CCM)wilaya misungwi mkoani mwanza kimewataka viongozi na wanachama wake kuyavunja makundi yaliyoibuka wakati wa mchakato wa kura za maoni za wenyeviti wa vitongoji,vijiji na mitaa pamoja na wajumbe wa serikali za mitaa na vijiji. Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Emmanuel Masangwa ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi na watendaji pamoja na wanachama wa chama hicho katika kata ya misasi. Masangwa amesema kuwa kuvunjwa kwa makundi hayo ni muhimu katika kukiwezesha chama hicho kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba 27 mwaka huu. ‘’Uchaguzi wa ndani wa chama chamapinduzi tumemaliza kufanya uchaguzi wetu,kwa hiyo tunaendelea kukiunganisha chama na kuendelea kuwaambia wanachama ambao hawakupata kura za kutosha waendelee kukiunga mkono CCM pamoja na viongozi ambao wameaminiwa ili kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa novemba 27’’alisema Masangwa na kuongeza kuwa ‘Kuwepo makundi wakati wa ucha...