Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Emmanuel Masangwa ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi na watendaji pamoja na wanachama wa chama hicho katika kata ya misasi.
Masangwa amesema kuwa kuvunjwa kwa makundi hayo ni muhimu katika kukiwezesha chama hicho kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba 27 mwaka huu.
‘’Uchaguzi wa ndani wa chama chamapinduzi tumemaliza kufanya uchaguzi wetu,kwa hiyo tunaendelea kukiunganisha chama na kuendelea kuwaambia wanachama ambao hawakupata kura za kutosha waendelee kukiunga mkono CCM pamoja na viongozi ambao wameaminiwa ili kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa novemba 27’’alisema Masangwa na kuongeza kuwa
‘Kuwepo makundi wakati wa uchaguzi ni Jambo la kawaida ambapo kila mmoja anakuwa na demokrasia yake ya kutafuta kura lakini baada ya kumaliza mchakato wetu wa ndani,kazi kubwa ambayo tunafanya ni kuunganisha wagombea wale waliopata nafasi ya kuongoza kwenye kura za maoni na wale ambao kura zao hazikutosha ili waweze kuwa kitu kimoja,CCM huwa hatuna mshindi kwenye kura za maoni bali huwa kura zinapungua’’
Masangwa amewataka wagombea ambao kura zao hazikutosha kuwaunga mkono wagombea walioteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho ili kukiwezesha chama kuibuka na ushindi wa kishindo.
Wakizungumza wakati wa kikao hicho,baadhi ya viongozi na wanachama wa ccm kata ya Misasi wamesema kuwa makundi yaliyopo kwenye kata hiyo ni ya kawaida ambapo wameahidi kuyavunja mara moja ili kuimarisha uhai wa chama.
‘’Sisi kama wanachama tunamuahidi mwenyekiti wa ccm wilaya pamaja na mkoa na Taifa kwa ujumla kuwa ccm misasi iko imara,makundi yaliyotokana na kura za maoni tumeshaamua kukaa meza moja ili tusiruhusu kuendelea kwa malumbano yanayoweza kuhatarisha ushindi wa chama’’walisema baadhi ya viongozi pamoja na wanachama wa ccm kata ya misasi













