Na Ada Shadrack, Nyamongo, Tarime. KAMPUNI ya dhahabu Barick North Mara, Nyamongo wilayani Tarime imetenga shilingi bilioni 9 katika kipindi cha mwaka 2024 ili kutekeleza Miradi 101 ya maendeleo kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo. Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa jana octoba 11 mwaka huu, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Apolinary Lyambiko alisema hayo na kufafanua kuwa miradi hiyo ni Afya, Elimu, miundombinu ya maji na shughuli nyingine za kijamii. "Katika kipindi cha mwaka 2022/2023 tumekamilisha miradi 115 ya maendeleo ya jamii iliyogharimu takriban Bilioni 7.3, pia kwa mwaka huu 2025 tumetenga Bilioni 9 kwa ajili ya kutekeleza wa miradi 101 ya huduma za kijamii."amesema. Lyambiko alisema awali kuwa utekelezaji wa huduma hizo ulikwama kutokana na mgongano wa kanuni za (CSR) ambapo tayari kampuni hiyo imeshafanya makubaliano na Halmashauri ya Tarime ambapo miradi imeanza kutekelezwa. Kwa upande wake Meneja Mahusiano wa Mgodi huo Francis Uhadi alitoa wito kwa v...
Marato tv - Sauti ya Jamii