Mbunge Mathayo atoa fursa kwa mafundi ujenzi,vigae na rangi

GEORGE MARATO TV
0



Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa Musoma mjini Vedastus Mathayo ametoa fursa ya kuwashika mkono mafundi wa ujenzi,Vigae, rangi ili kusoma Veta Mara na kupata cheti.

Fursa aliyoitangaza Mathayo ni kuchangia sehemu ya gharama na kujifunza chuoni hapo.

Kauli hiyo ameitoa leo oktoba 11 wakati akikabidhi vyeti kwa wahitimu 67 wakiwemo makatibu wa CCM wa Kata Musoma mjini waliosoma chuoni hapo.

Amesema Veta Mara imetangaza mafunzo ya muda mfupi na kupunguza gharama baada ya ombi alililowafikishia na yeye kwa watakaojitokeza kujifunza atawashika mkono.

Mbunge huyo amesema serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inaleta fedha nyingi kwa miradi ya ujenzi na walio na vyeti vya mafunzo kutoka Veta wanapewa nafasi ya kushiriki ujenzi wa miradi hiyo.

" Leo tunamalizana na waliopata mafunzo ya kuendesha pikipipiki wakiwemo viongozi wa Chama na sasa naitangaza fursa nyingine.

" Mafundi wa fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapa niko tayari kuwashika mkono kujifunza na kupata vyeti vitakavyowawezesha kupata kazi za miradi ya serikali ",amesema

Mkuu wa chuo cha Veta Mara Moleli Moleli amesema Mbunge Mathayo amekuwa akiwapenda wananchi anaowaongoza na amekuwa akiwapigania kwa masuala muhimu.

Amesema kwa mafunzo hayo yaliyokuwa yakitolewa kwa miezi 5 kwa gharama ya shilingi laki 5,50,000 sasa yatatolewa kwa kipindi kifupi cha mwezi 1 kwa gharama ya shilingi laki 1,80000 kabla haujaingizwa udhamini wa mbunge.



 



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top